Timu ya Kagera sugar imeuzindua rasmi uwanja wa Kaitaba kwa kupata ushindi wa goli moja dhidi ya Mwadui Shinyanga,Awali kabla ya mchezo kuanza Mkuu wa Mkoa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Kijuu alipata wasaa wa kukagua uwanja kujionea namna ukarabati ulivyofanyia na aliuzindua kwa kupiga penati kuashilia kuufungua rasmi,Uwanja wa Kaitaba umezinduliwa rasmi baada ya kukarabatiwa na FIFA kwa asilimia mia moja,Changamoto iliyopo sasa ni namna ya kuboresha miundo mbinu ya uwanja yakiwemo majukwaa ili hali halisi iweze kwendana na adhi ya uwanja.Hafla ya ufunguzi iliudhuriwa na uongozi wa juu wa TFF , akiwemo makamu mwenyekiti, katibu mkuu, viongozi wa kanda na Mkoa.
Mkuu wa mkoa akipiga penati, kuashilia ufunguzi wa uwanja wa Kaitaba.
Kushoto ni Al Amin Abdul Katibu msaidizi KRFA akiwa na shabiki nguli wa Kagera sugar Bw Mwinyi.
Makamu mwenyeti TFF Bw Kalya akitoa maelezo kwa mgeni rasmi.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera mwenye Track suite akipata maelezo kwa mtaalamu anaeendesha mashine maalumu ya nyasi bandia.
Kushoto ni afisa utamaduni Manispaa Bukoba Rugeiyamu akiteta na Bw Yahaya.
Mgeni rasmi akikagua maeneo ya viongozi wa timu wanapokaa.
Waandishi wa habari.
Bw Yahaya, mwenyekiti wa vilabu ambae pia ni Mkurugenzi wa kiwanda cha sukari Kagera na Mtibwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uboreshaji wa miundo mbinu ya uwanja wa Kaitaba(Huu uwanja ni wa Manispaa, kwa hiyo hatuna mamlaka nao,tutafanya mazungumzo kuona tunaweza kusaidia vipi.)
Mashabiki wa Kagera sugar wakishangilia.
Mgeni rasmi akiongea na wachezaji.
No comments:
Post a Comment