Saturday, 17 August 2013

FOOLISH AGE YA LULU KUZINDULIWA MWISHO WA MWEZI HUU NDANI YA MLIMANI CITY


  Msaani mwenye kipaji cha Hali ya juu nchini na Mwenye umri mdogo Elizabeth Michael "LULU"anatarajia kuzindua filamu yake ya Kwanza tokea alipotoka Gerezani, Filamu hii iitwayo FOOLISH AGE ikiwa imetengezwa na Kampuni ya Proin Promotion Limited itazinduliwa Mnamo tarehe 30 August.

 2013 Katika Ukumbi wa Mlimani city jijini Dar Es Salaam. Filamu hiyo inayoelezea Maisha ya LULU ni moja ya filamu nzuri na yenye ubora wa hali ya juu kutokana na Kutengenezwa na Kampuni ya Proin Promotion Limited Katika Uzinduzi huo wa Filamu hiyo ya Lulu Wasanii mbalimbali akiwemo mwanamuziki Lady Jaydee na Machozi Band anatarajiwa kushusha bonge moja la burudani ya kufa mtu. 

Kupitia mtandao wa kijamii wa Lulu aliyejaaliwa kuwa na kipaji cha kuigiza na mwenye mvuto mbele ya runinga aliandika "Nina kila sababu ya kumshukuru Mungu....!!!ninafuraha ya kuwafahamisha kuwa TAREHE 

30/8/2013 ndio siku nitakayozindua movie yangu mpya iitwayo FOOLISH AGE....Hatimaye narudi kazini!!!!Uzinduzi utafanyika katika ukumbi wa MLIMANI CITY....kutakuwepo na wasanii mbalimbali wa muziki....na pia LADY JAY DEE pamoja na MACHOZI BAND atakuwepo pia!!!nahitaji support ya mashabiki wote wa LULU na mashabiki wa BONGO MOVIE.....♥♥♥♥!!!#PROINPROMOTERS"

Baada ya uzinduzi wa Filamu hii nakala zitaendelea kuuzwa katika maduka yote ya Filamu nchini na Filamu hii imetengenezwa na itakuwa inasambazwa na Kampuni ya Proin Promotion Limited
Usikose uzinduzi Huu utakaofanyika ndani ya Ukumbi wa Mlimani City tarehe 30 August 2013

YANGA YATWAA NGAO YA HISANI


Saturday, August 17, 2013





Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mecky Sadiq Mecky akimkabidhi Nahodha wa Yanga ngao ya jamii baada ya kuifunga Azam FC bao 1-0 katika mchezo uliochezwa Taif




Friday, 16 August 2013

KAGASHEKI CUP 2013: KITENDAGURO 3 vs KASHAI FC 1, HATUA YA NUSU FAINALI YAMALIZIKA LEO, KESHO FAINALI


Waamuzi wa mtanange huu wa leo kati ya Kitendaguro na Kashai

Kikosi cha Kashai kilichoanza
Kikosi cha Kitendaguro na kiongozi wao (kulia)

Mtanange ukiendelea..........

Wachezaji wa Kitendaguro maarufu kama Makhirikhiri wakionesha kutawala uwanja kipindi chote cha kwanza na kuwafunga bao zote tatu kwenye kipindi cha dakika 45.

Wachezaji wa Kitendaguro kushoto wakishangilia baada ya kupata bao la kwanza na la mapema huku kulia wachezaji wa Kashai Fc wakilalamika kwamba siyo bao wameotea!!

Wachezaji wa Kitendaguro wakishangilia baada ya kupata bao la pili

Mashabiki wa Kashai Hoi..wakionekana kuwa wapole!!!

Mchezaji wa Kitendaguro akitaka kukatiza mbele ya mabeki wa Kashai Fc

Mtanange ukiendelea..Kiongozi wa timu ya Kashai akiondolewa nje ya uwanja baada ya kumjia juu mwamuzi wa mchezo huu baada ya timu ya Kashai kufungwa bao la kwanza


Mashabiki

Mashabiki wa Kashai leo walikuwa hwana raha kabisa kutokana na kichapo cha juzi na dalili za kuonekana kuchapwa tena leo!!! mashabiki walikuwa hawana raha na kikosi chao!!

Kiongozi wa Timu ya Kashai akiondolewa nje ya uwanja baada ya kuleta shida kwa mwamuzi mapema kipindi cha kwanza.
Nje!!
Abdulzack kushoto na kulia ni Dj Y wakitangaza mtanange huo live Radio Kasibante Fm 88.5
RATIBA: HATUA YA  FAINALI
Jumanne 13 Agosti
10:00 Jioni  - Bilele  1 v/s kitendaguro 0
Jumatano 14 Agosti
10:00 Jioni - Kashai Fc 1 v/s  Rwamishenye Fc 2
Ijumaa 16 Agosti
Kutafuta mshindi wa tatu, itakuwa ni:-
Kitendaguro Fc 3 v/s Kashai Fc 1

Jumamosi 17 Agosti 
FAINALI
Bilele fc v/s Rwamishenye fc

AKAMATWA NA MENO YA TEMBO YENYE THAMANI YA MILIONI 23.2 JIJINI MWANZA


 MKAZI wa Kijiji cha Buhemba Wilaya ya Butiama Mkoani Mara Yohana Jackison (27) amekamatwa na Askari Polisi wa dolia akiwa na vipande 10 vya meno ya Tembo vyenye thamani ya zaidi shilingi milioni 23.2 Jijini Mwanza.
Gunia lililokamatwa na nyaraka hizo za serikali (meno ya Tembo).
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Evarist Mangu jana alieleza kuwa mtuhumiwa huyo aliyekuwa akisafirisha meno ya tembo kutoka kijiji cha Buhemba kuja Jijini Mwanza alikamatwa na askari wa dolia katika Kituo Kikuu cha Mabasi cha Buzuruga majira ya saa 3:15 asubuhi kwenye kilichopo eneo la Nyakato baada ya kushitukiwa na askari hao.
Kamanda Mangu alisema kwamba baada ya kushuka kwenye basi dogo mali ya Kampuni ya JOHANVIA Express linalofanya safari zake kati ya Butiama na Mwanza akiwa ameficha vipande vya meno hayo ya Tembo kwenye gunia la mkaa ambapo baada ya kutelemka na kuonyesha wasiwasi ndipo askari hao waliamua kumsimamisha.
Vipande vya meno ya Tembo vikikaguliwa mara baada ya kutolewa kwenye gunia.
Yohana Jackison (27)

MWAKYEMBE AWATAJA WAHUSIKA WA DAWA ZA KULEVYA




Thursday, 15 August 2013

RASTA ADAKWA NA DAWA ZA KULEVYA UWANJA WA NDEGE DAR



Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe akionesha picha ya kijana Leonard Jeremiah Monyo ( Edwin Jeremiah Monyo) ambaye amekamatwa na kete 86 za madawa ya kulevya aina ya heroine.
Kijana Leonard Jeremiah Monyo ( Edwin Jeremiah Monyo) ambaye amekamatwa na kete 86 za madawa ya kulevya aina ya heroine.
Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe akizungumza na vyombo vya habari leo.
JUHUDI za Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe za kupambana na dawa za kulevya nchini Tanzana zimeanza kuzaa matunda baada ya jana akiwa katika ukaguzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa Julius Nyerere kunaswa kijana akijaribu kupita na dawa za kulevya katika uwanja huo.
Kwa kile kuoneshwa kukerwa na tabia hizo, Dk. Mwakyembe amempiga picha kijana huyo ambaye ni rasta na pita yake itasambazwa maeneo tofauti, huku kesi yake ikiendelea ya kupatikana na madawa hayo ya kulevya.

Akizungumza na vyombo vya habari leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Dk. Mwakyembe alimtaja kijana aliyekamatwa jana kuwa ni Leonard Jeremia Monyo (Edwin Jeremiah Monyo) ambaye amekamatwa na kete 86 za madawa ya kulevya aina ya heroin akitaka kusafiri nazo kuelekea misokoto ya bangi 34 akiwa ameficha kwenye begi lake.

Alisema kijana huyo rasta alinaswa na mtambo wa kukagua mzigo baada ya wakaguzi kuushuku mzigo wake hivyo kuamuru ukaguliwe ndipo alipokutwa na madawa hayo haramu akijaribu kusafiri nayo kwa ndege.

Badhi ya wanahabari wakimsikiliza Dk. Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe
Alisema kijana huyo kwa sasa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa uchunguzi zaidi kabla ya kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya kukutwa na dawa hizo haramu. Alisema kwa kile kuoneshwa kukerwa na vitendo hivyo na kuamua kwa dhati kupambana navyo wamempiga picha kijana huyo na picha zake zitasambazwa maeneo mbalimbali ili aonekane na umma kujua watua ambao wamekuwa wakilichafua taifa nje na ndani kutokana na biashara hizo haramu.
Dk. Mwakyembe amesema atahakikisha anafuatilia kesi ya kijana huyo hadi itakapoishia ili uona hatua za kisheria zinachukuliwa kwa wahusika na vitendo hivyo kukomeshwa. Alisema maofisa wakaguzi wa mizigo wawili (wote wasichana) ambao walimnasa kijana huyo watazawadiwa na kupandishwa daraja kutokana na kazi nzuri waliyoifanya.

“Jana tu baada ya ukaguzi wenzetu ambao wanaona kama tunafanya mzaha jana tena wakapitisha mzigo wa madawa ya kulevya kiwanja cha ndege cha Dar es Salaam, kwa sababu vijana wetu sasa wameamka na hawataki mchezo wakamkamata kijana huyo…,” alisema.

“Picha yake itasambazwa kila sehemu…sidhani kama tunahitaji upelelezi kwa sababu tumekukamata na dawa za kulevya. Mimi na viongozi wangu kupitisha dawa za kulevya akikisha kuuhakikisha.

Alisema kijana huyo alikamatwa majira ya saa mbili na nusu usiku akiwa anasafiri kwenda nchini Italia kwa kutumia ndege ya kampuni ya Swissair. Alisema kwa sasa kila atakayekamatwa na dawa za kulevya picha yake itasambazwa maeneo mbalimbali ya nchi ili watu hao wajulikane.

Alisema kwa sasa taratibu zinafanywa ili kuhakikisha mizigo ya abiria wanaowasili kutoka nje ya nchi kuingia Tanzania nao mizigo ikaguliwe ili kuwabaini wanaoingiza bidhaa hiyo haramu ichini pia. Aliongeza zoezi hilo litafanyika katika viwanja vya ndege na bandarini kwa kila mizigo inapowasili.

Alisema lengo ni kuhakikisha viwanja vya ndege vinakuwa salama na kuacha kutumika vibaya na baadhi ya watu, jambo ambalo limeendelea kulichafua taifa. Alisem kiwanja cha Dar es Salaam ni kizuri na kina vifaa vya usalama vya kutosha ila mapungufu yaliyopo ni kwa baadhi ya wafanyakazi ambao wanatumia vibaya madaraka yao.

Dk. Mwakyembe ameahidi kuwataja na kuweka picha zao hadharani watu ambao wanajihusisha na madawa hayo ya kulevya. Amesema wanatarajia kutaja majina ya Watanzania ambao hivi karibuni walinaswa na dawa za kulevya nchini Afrika Kusini katika uwanja wa ndege wa Oliver Tambo. Alisema Watanzania wengine wamekamatwa Hong Kong wakihusishwa na dawa hizo na wanafuatilia pia picha na majina yao yatawekwa hadharani muda wowote
.

APEWA Tshs 120.000 KUTOROSHA TWIGA UWANJA WA KIA



Shahidi wa 10 katika kesi ya usafirishaji wanyama hai nje ya nchi amemtaja mshitakiwa wa kwanza, Kamran Mohamed, ambaye ni raia wa Pakistan kuwa alimzawadia Sh. 120,000 kwa ajili ya kazi aliyoifanya ya kupakia wanyama hao kwenye ndege ya Qatar Airforce Novemba 25, 2010.

Akitoa ushahidi wake mbele ya Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Kobelo, shahidi huyo ambaye ni mfanyakazi wa Kampuni ya Swissport International inayohudumia mizigo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), Ally Mzava, alidai mahakamani kuwa siku hiyo alipewa taarifa kuwa kutakuwa na ndege ya dharura.

Kwamba, ndege hiyo itafika KIA usiku na kupakia ndege, hivyo alitakiwa kuwataarifu wenzake ili wawe tayari kwa ajili ya kupakia wanyama hao.


Mzava alidai kuwa mara baada ya kupewa taarifa hiyo kutoka kwa mkuu wa kitengo cha ndege za dharura aliyemtaja kwa jina la Rosemary Michael, aliwaandaa wenzake na baada ya ndege hiyo kufika KIA, walianza kupakia mizigo hiyo, ambayo ilikuwa imefungwa kwenye maboksi.

“Tuliifanya kazi hiyo kwa umakini. Tukiwa ndani ya ile ndege pale pale uwanjani, nilipewa Sh. 120,000 kama ‘tip’ (bakshishi) ya kazi tuliyoifanya na kuambiwa na Mhindi aliyekuwamo mle ndani kuwa nigawane na wenzangu…ninamfahamu ni yule Mhindi pale nasikia wanamwita Kamran,” shahidi huyo aliiambia mahakama.

Alidai baada ya kumaliza kazi hiyo, aliondoka na hakujua kilichoendelea kutokana na kazi aliyotakiwa kuifanya kukamilika.

Shahidi huyo alidai ndege hiyo ilikuwa imeandikwa ubavuni jina la Qatar Airforce One.
Shahidi mwingine, Joseph Mpimbwe, ambaye ni msimamizi katika Kampuni ya Swissport iliyopewa dhamana ya kupakia na kushusha mizigo kwenye ndege KIA, alidai aliona twiga wawili wakipakiwa kwenye ndege.

Mbele ya Hakimu Kobelo, shahidi huyo alidai katika tarehe hiyo alipigiwa simu na Rosemary na kupewa taarifa ya kuwapo kwa ndege itakayosafirisha wanyama usiku wa manane. Alidai kuwa baada ya kupigiwa simu hiyo, alimpigia simu Moris Njau na kumpa taarifa hiyo ili awaandae wafanyakazi wenzake kwa ajili ya upakiaji wa wanyama hao.

“Nilipata bahati ya kuona twiga wawili wakiwa wamefungwa kwenye boksi na kulikuwa na vifurushi vingi vilivyokuwa vimefungwa. Siyo mara ya kwanza kupakiza wanyama,” aliiambia mahakama na kuongeza:

“Na tumekuwa tukifanya hivi mara kwa mara, ndege iliondoka kesho yake asubuhi baada ya sisi kumaliza kupakia wanyama hao. Ilikuwa saa 12:00 kasoro,” alidai.

Hata hivyo, shahidi huyo alidai hawawezi kupakia mzigo kwenye ndege bila ya kuwa na kibali kinachoeleza aina ya mzigo, uzito wake na anayehusika nao (cargo manifest), ambayo inaelezea aina ya mzigo unaopaswa kupakiwa au kushushwa kwenye ndege.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 24, mwaka huu mashahidi wengine watakapoendelea kutoa ushahidi wao.

Wanyama hao wanadaiwa kutoroshwa kwa kutumia ndege ya Quatar Emiri Air Force kwenda Doha, nchini Qatar, Falme za Kiarabu kupitia KIA. Inadaiwa kuwa wanyama aina tofauti 144 na ndege pori wawili.

Katika orodha hiyo, inadaiwa kuwa kulikuwa na twiga na viroba vya nyama pori ya kukausha zaidi ya tani tano.

Utoroshaji huo unadaiwa kuwa uliikosesha serikali zaidi ya Sh. milioni 170. Ilidaiwa kuwa wanyama hao walipakiwa usiku wa manane Novemba 24, 2010 na kuwa kampuni ya uwindaji wanyama ya Ham Marketing na Kampuni ya Uwindaji Ndege ya Luwego Bird Trappers ndizo zilizokamata wanyama hao na ndege
.

CCM MKOA KAGERA NI MAJANGA.... MWENYEKITI WA CCM MKOA CONSITANCIA BUHIYE ATUNISHA MSULI ASEMA HAJASIKIA TAMKO LA NAPE NA HALIHUSIANI NA MAAMUZI YA HALMASHAURI KUU YA MKOA YA KUWAFUKUZA MADIWANI WANANE

 Muda mfupi uliopita mwenyekiti wa mkoa wa kagera ccm constansia buhiye ameita waandishi wa habari na kuongea nao katika ukumbi wa mkutano wa ccm mkoa na  kusisitiza kuwa maamuzi yaliyotolewa na halmashauri kuu ya mkoa ya kuwafukuza na kuwaondolea nyadhifa za udiwani madiwani wanane wa chama mapinduzi manispaa ya bukoba,maamuzi yako palepale,akijibu baadhi ya maswali yaliyoulizwa na waandishi wa habari kuhusiana na tamko la katibu mwenezi taifa ndugu Nape kutengua maamuzi ya halmashauri kuu ya mkoa wa kagera,mwenyekiti amesema hata taarifa ya Nape hajaisikia, anacoeleza ni maamuzi waliyoyafanya kwa mujibu wa katiba ya chama, kauli  ya mwenyekiti ilizua maswali mengi kwa waandishi na kusababisha kuleta picha ya kauli za viongozi kupingana na kuchanganya wananchi kushindwa kuelewa kauli ya nani na yupi ni sahihi.
mwenyekiti wa ccm mkoa akiongea na waandishi wa habari leo kususitiza kuwa  maamuzi ya halmashauri kuu ya mkoa dhidi ya madiwani  wanane wa ccm bukoba mjini ndio sahihi
                              waandishi wa habari wakisikiliza maelezo ya mwekiti ccm mkoa wa kagera
                                       waandishi wakiwa makini kuandika anachoeleza mwenyekiti
kauli ya mwenyekiti imeonyesha alichozungumza Nape ni maswala binafsi,maamuzi waliyoamua halimashauri kuu mkoa ndio sahihi,na mkweli,nani msemaji  wa chama,yote hayo ni maswali  yanasubiri majibu
                                                                Endelea kufutilia jamcoblogspot.blogspot.com