Wednesday 14 August 2013

POLISI WAKAMATA MAGUNIA 405 YA BANGI ARUMERU


Katika Operesheni ya Kuzuia Uhalifu na Madawa ya Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha liliingia kijijini hapo majira ya saa 2 za asubuhi Agosti 13 mwaka huu.

Ilikuwa ni ziara ya kushtukiza katika kijiji hicho hali iliyowafanya wanakijiji kutaharuki na kuanza kukimbia na kutokomea milima wakiziacha nyumba zao zikiwa wazi.

Uongozi wa Kijiji hicho nao ulitoweka kusikojulikana kwa kuhofia mkono wa Jeshi la Polisi.
Kamishna wa Operesheni hiyo ACP Ngonyani alisema safari hii waliamua kwenda baada ya mavuno kutokana na ukweli kwamba zikiwa bado shamabni ni kazi nzito sana ya kufyeka.

ACP Ngonyani aliongeza kusema magunia 225 ya zao hilo haramu nchini Tanzania waliamua kuyateketeza kutokana na namna ya kuyasafirisha kuwa mgumu.

Mkuu wa Operesheni hiyo alisema operesheni hiyo bado ni endelevu katika kijiji hicho kwa mwaka huu ni mara ya pili lakini wamegundua mbinu mpya.

Pia alisema magunia 127 na watuhumiwa watano wamewasafirisha hadi makao makuu kwa hatua zaidi za kisheria.

Wanakijiji wameilalamikia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jeshi la Polisi kuwa zao hil ni muhimu kwa familia zao kwani wanapoliuza husomeshea watoto wao na mahitaji mengine ya kifamilia.

katika operesheni hiyo ilishuhudia nyumba moja ya kijana wa kidato cha Nne  ikiwa na magunia mawili ya Bangi na baada ya uchunguzi zaidi mwanafunzi huyo alidai kuwa alivuna ili auze akalipe ada na mahitaji mengine ya kifamilia.

Imebainika kwamba guni moja linapouzwa kutoka shambani hutoa kiasi cha zaidi ya shilingi 100,000/= za Tanzania.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha Liberatus Sabas amewataja watuhumiwa waliokamatwa katika operesheni hiyo ambayo imevunja rekodi ya zilizopita kuwa ni Nemali Saitoti (50), Esuba Daudi (33), Thomas Lesnoi (63), Lomayan Thomas (27) na Natumi Daudi (29). 

ACP Sabas amesema opersheni hiyo ni endelevu na amewataka wananchi, wakulima na watumiaji kuacha kuendeleza zao hilo kwani ni kinyume cha sheria huku akiwataka kuendeleza Polisi Jamii na Ulinzi Shirikishi.

No comments:

Post a Comment