Muda mfupi uliopita mwenyekiti wa mkoa wa kagera ccm constansia buhiye ameita waandishi wa habari na kuongea nao katika ukumbi wa mkutano wa ccm mkoa na kusisitiza kuwa maamuzi yaliyotolewa na halmashauri kuu ya mkoa ya kuwafukuza na kuwaondolea nyadhifa za udiwani madiwani wanane wa chama mapinduzi manispaa ya bukoba,maamuzi yako palepale,akijibu baadhi ya maswali yaliyoulizwa na waandishi wa habari kuhusiana na tamko la katibu mwenezi taifa ndugu Nape kutengua maamuzi ya halmashauri kuu ya mkoa wa kagera,mwenyekiti amesema hata taarifa ya Nape hajaisikia, anacoeleza ni maamuzi waliyoyafanya kwa mujibu wa katiba ya chama, kauli ya mwenyekiti ilizua maswali mengi kwa waandishi na kusababisha kuleta picha ya kauli za viongozi kupingana na kuchanganya wananchi kushindwa kuelewa kauli ya nani na yupi ni sahihi.
mwenyekiti wa ccm mkoa akiongea na waandishi wa habari leo kususitiza kuwa maamuzi ya halmashauri kuu ya mkoa dhidi ya madiwani wanane wa ccm bukoba mjini ndio sahihi
waandishi wa habari wakisikiliza maelezo ya mwekiti ccm mkoa wa kagera
waandishi wakiwa makini kuandika anachoeleza mwenyekiti
kauli ya mwenyekiti imeonyesha alichozungumza Nape ni maswala binafsi,maamuzi waliyoamua halimashauri kuu mkoa ndio sahihi,na mkweli,nani msemaji wa chama,yote hayo ni maswali yanasubiri majibu
Endelea kufutilia jamcoblogspot.blogspot.com
No comments:
Post a Comment