Saturday 24 January 2015

KAMATI TENDAJI YA KRFA YAFANYA KIKAO NA RAIS WA TFF JAMAL MALINZI ATEMBELEA UWANJA WA KAITABA KUJIONEA MAENDELEO YA UWEKAJI NYASI BANDIA.

 Mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu Mkoa wa Kagera (KRFA) Jamal Emil Malinzi akiwa na kamati tendaji wametembelea uwanja wa Kaitaba na kujiona jinsi unavyoendelea kutengenezwa kwa ajiri ya kuwekewa nyasi bandia,mara baada ya kuwasili Bw Jamal ambae pia ni rais wa shirikisho la chama cha mpira wa miguu Tanzania (TFF) alikutana na mtaalamu kutoka FIFA anaesimamia zoezi zima la maandalizi ya uwekaji wa nyasi  bandia Bw  Doron Mommsen alimueleza zoezi linavyoendelea na nini kitafanyika mpaka kufikia hatua ya uwekaji wa nyasi bandia,Baada ya maongezi hayo Bw Jamal alitoa rai kwa viongozi wa serikali na wote watakaokuwa na mamlaka na uwanja wa Kaitaba kuhakikisha mara utakapomalizika kutengenezwa kuutunza na kuusimamia ili uweze kudumu kwa muda mrefu,Amesema uwanja wa Kaitaba kwa asilimia mia moja unagharamiwa na FIFA baada ya yeye (Jamal Malinzi) kuuombea maombi maalumu FIFA na wakakubari kuutengeneza.
 Mapema kabla ya kutembelea uwanja kilianza kikao cha kamati tendaji ya KRFA kikiongozwa na mwenyekiti wake Jamal Malinzi katika ukumbi wa hotel ya Victorius Peach.
 Bw Jamal akiwa na katibu wake Bw Umande Chama,ambae pia ndio mwenyekiti wa wahamuzi TFF.
 Kushoto ni Bw Pelegrius .A. Rutayuga mjumbe wa kamati tendaji KRFA na  pia ni mshauri mkuu wa kiufundi TFF makao makuu.
 Kulia ni Bw Rugeiyamu  Afisa utamadunu Manispaa ya Bukoba.
 Mjumbe kutoka Ngara.
 Bw Jamco na Bw Wily mkurugenzi wa kampuni mpya ya utalii Bukoba Tour wakiteta jambo uwanja wa Kaitaba.

 Kushoto ni blogger wa Bukobasports Faustine Ruta akiwa na Bw Willy.
 Bw WILLY kikazi zaidi akiitangaza kampuni yake kwa mtaalamu wa uwekaji nyasi bandia kaitaba kutoka FIFA.
 Mtaalamu anaesimamia kuweka nyasi bandia akimkaribisha Mwemyekiti wa KRFA Jamal Malinzi na ujumbe aliofuatana nao.
 Akipata maelezo maendeleo ya  utengenezaji uwanja.
 Wanategemea kufikia mwezi wa nne mwaka huu kuwa wamekamilisha uwekaji wa nyasi bandia na miundo mbinu yote ya kuhakikisha maji hayatuami katika uwanja.
 Picha ya pamoja.

 Akasisitiza Jamal Malinzi kuutunza uwanja ukikamilika.
Mwenyekiti wa KRFA Jamal Malinzi  akiwa na baadhi ya wajumbe wa kamati tendaji,katika picha ya pamoja mbele ya kifaa kinachotumika kutengeneza uwanja wa kaitaba.

RAIS ABADILI MAWAZIRI NA MANAIBU WAO, WAPO HAPA WOTE



 
Waziri wa Nishati na Madini mpya, George Simbachawene.
Waziri wa Afrika Mashariki, Dk. Harrison Mwakyembe.
Waziri wa Mahusiano na Uratibu, Mary Nagu.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi, Wiliam Lukuvi.
Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Steven Wassira.
 
Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji, Christopher Chiza.
 
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano, Steven Masele.
 
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi, Angellah Kairuki.
 
Naibu Waziri Katiba na Sheria,Ummy Mwalimu.
 
Naibu Waziri Anna Kilango Malecela, Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amebadili mawazini na naibu mawaziri Ikulu leo.
Akitangaza mabadiliko ya mawaziri hao leo, Katibu Mkuu Kiongozi wa Ofisi ya Rais,  Sifue Ombeni alitaja mawaziri hao wapya ambao wanaapishwa jioni hii na wizara zao kwenye mabano kuwa George Simbachawene (Nishati na Madini), Mary Nagu (Mahusiano na Uratibu), Dk. Harrison Mwakyembe, (Afrika Mashariki).
Wengine ni Wiliam Lukuvi (Ardhi, Nyumba na Makazi), Steven Wassira (Kilimo Chakula na Ushirika), Samwel Sitta (Uchukuzi), Jenista Mhagama (Sera na Uratibu wa Bunge) na Christopher Chiza (Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji).
Rais pia ameteua manaibu waziri na wizara zao kwenye mabano kama ifuatavyo: Steven Masele (Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano), Angellah Kairuki (Ardhi Nyumba na Makazi), Ummy Mwalimu (Katiba na Sheria), Anna Kilango Malecela (Elimu na Mafunzo ya Ufundi), Charles Mwijage (Nishati na Madini).

Friday 23 January 2015

BEI YA NDIZI SOKO KUU BUKOBA YASHUKA,ANGALIA MATUKIO TOFAUTI KATIKA PICHA.

 Hali ya ndizi katika soko kuu la Bukoba,Siku za hivi karibuni palikuwepo na uhaba wa ndizi na mfumuko wa bei kubwa ya ndizi kati ya elfu kumi na thelasini elfu kwa ndizi mmoja,hali ambayo leo tumekuta ni  tofauti,Ndizi zimefurika na bei ni kati ya  elfu tano na kumi na tano elfu.Hali hii imekuwa faraja kwa wakazi wa Manispaa na maeneo mengine kwa kuweza kujipatia ndizi kwa bei nafuu.



 Bi Asia, mfanyabiashara wa ndizi ,soko kuu Bukoba.
 Hali iko hivi.
 Vijana kazini ,soko kuu Bukoba.
 Mmmoja ya wafanyabiashara ya ndizi soko kuu Bukoba,alieleza namna ndizi zilivyoshuka bei kwa kiwango kikubwa,na alisema kwa sasa  ndizi nyingi zinatoka nchini Uganda,kitu ambacho kimechangia ushukaji wa bei ya ndizi.
 Ni mmoja wa wadada  wa Jamcobarber shop,karibu.Ni moja ya saloon ya kisasa ,yenye viwango na ubora.
 Bw AMIRALI'S wauzaji wa vifaa vya ujenzi kwa gharama nafuu, wapo Miembeni,karibuni.
 Bw Zuri akiwa dukani kwake, fika uone ,yupo Miembeni.
 Yunis Ruangisa akiwa na Teddy Mboto,wakiwa kazini,wadau wakubwa wa jamcoblog.
 Mama Mzee akiwa kazini dukani kwake SOKO KUU ndani Bukoba.
 Wadau wakubwa wa jamcoblog.
 Mdau Jamal Issa akiwa kidigital zaidi.
 Karibu upate pikipiki ya viwango kwa RMK, Mtaa wa Migeyo.
 Bi Sauda Kichwabuta akiwa kazini,wauzaji wa pikipiki , wapo mtaa wa Migeyo au  uliza kwa kijana makini RMK au Ramadhani Kambuga ambae yuko mapumziko nchini Sweden.
 Migeyo hiyooo.
 Hajat,mmoja ya wafanyakazi makini sana wa Mdau Rukia Mawenya kwenye moja ya duka lake la Mpesa  mtaa wa Migeyo.
 Camera yetu inakutana na chui na London mida ya jioni baada ya kazi dukani kwa Alipenda wakiongea.
 Azam ni shidaaa, Dukani kwa Mitesh wakishusha mzigo.
 Kulia ni mdau  mkubwa wa jamcoblog, Bw Yunus Kabyemela , na mdogo wake Mzakiru.
 Maeneo ya kwa Mushamu.Bw  musa  , mwenye miwani  mchezaji mstaafu wa timu ya Bohari  Kagera miaka ya themanini,kwa sasa veterani Dodoma akiwa kwa Bw Mushamu mmoja wa wachezaji  wa wazamaji wa RTC KAGERA.
 Pande za Miembeni Bukoba.
 Mtaa wa Diwani kata ya Miembeni utajipatia vitanda vizuri kwa gharama ya chini, karibuni  sana waunge mkono vijana wajasiriamali wanaojituma na uwezo mkubwa wa kufanya kazi.
 Pande za Saloon ya kisasa Jamcoberber shop,fika upate huduma zao.
 Liberata akiwa na mme wake Bw Manyere wakipata chakula.wakiwa nyumbani kwa familia ya Jamal Kalumuna,walifika kuwapo pole ya matatizo ya kuvamiwa na watu wanaosadikiwa ni majambazi hivi karibuni.
 Bw Romward Bashereka akiwa na mama Rama.
 Ni wageni walioitembelea familia ya Jamal Kalumuna (jamco) kuwapa pole ya matatizo yaliyowakuta hivi karibuni ya kuvamiwa na watu wanaosadikiwa ni majambazi.
 Mr Manyere akiongea kitu fulani kwa msisitizo.
 Ni katika kuongea mawili matatu.
 Bi Liberata Bashereka katika pozz.
Angali jamcobukoba.blogspot.com kwa habari za uhakika.