Saturday 24 January 2015

KAMATI TENDAJI YA KRFA YAFANYA KIKAO NA RAIS WA TFF JAMAL MALINZI ATEMBELEA UWANJA WA KAITABA KUJIONEA MAENDELEO YA UWEKAJI NYASI BANDIA.

 Mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu Mkoa wa Kagera (KRFA) Jamal Emil Malinzi akiwa na kamati tendaji wametembelea uwanja wa Kaitaba na kujiona jinsi unavyoendelea kutengenezwa kwa ajiri ya kuwekewa nyasi bandia,mara baada ya kuwasili Bw Jamal ambae pia ni rais wa shirikisho la chama cha mpira wa miguu Tanzania (TFF) alikutana na mtaalamu kutoka FIFA anaesimamia zoezi zima la maandalizi ya uwekaji wa nyasi  bandia Bw  Doron Mommsen alimueleza zoezi linavyoendelea na nini kitafanyika mpaka kufikia hatua ya uwekaji wa nyasi bandia,Baada ya maongezi hayo Bw Jamal alitoa rai kwa viongozi wa serikali na wote watakaokuwa na mamlaka na uwanja wa Kaitaba kuhakikisha mara utakapomalizika kutengenezwa kuutunza na kuusimamia ili uweze kudumu kwa muda mrefu,Amesema uwanja wa Kaitaba kwa asilimia mia moja unagharamiwa na FIFA baada ya yeye (Jamal Malinzi) kuuombea maombi maalumu FIFA na wakakubari kuutengeneza.
 Mapema kabla ya kutembelea uwanja kilianza kikao cha kamati tendaji ya KRFA kikiongozwa na mwenyekiti wake Jamal Malinzi katika ukumbi wa hotel ya Victorius Peach.
 Bw Jamal akiwa na katibu wake Bw Umande Chama,ambae pia ndio mwenyekiti wa wahamuzi TFF.
 Kushoto ni Bw Pelegrius .A. Rutayuga mjumbe wa kamati tendaji KRFA na  pia ni mshauri mkuu wa kiufundi TFF makao makuu.
 Kulia ni Bw Rugeiyamu  Afisa utamadunu Manispaa ya Bukoba.
 Mjumbe kutoka Ngara.
 Bw Jamco na Bw Wily mkurugenzi wa kampuni mpya ya utalii Bukoba Tour wakiteta jambo uwanja wa Kaitaba.

 Kushoto ni blogger wa Bukobasports Faustine Ruta akiwa na Bw Willy.
 Bw WILLY kikazi zaidi akiitangaza kampuni yake kwa mtaalamu wa uwekaji nyasi bandia kaitaba kutoka FIFA.
 Mtaalamu anaesimamia kuweka nyasi bandia akimkaribisha Mwemyekiti wa KRFA Jamal Malinzi na ujumbe aliofuatana nao.
 Akipata maelezo maendeleo ya  utengenezaji uwanja.
 Wanategemea kufikia mwezi wa nne mwaka huu kuwa wamekamilisha uwekaji wa nyasi bandia na miundo mbinu yote ya kuhakikisha maji hayatuami katika uwanja.
 Picha ya pamoja.

 Akasisitiza Jamal Malinzi kuutunza uwanja ukikamilika.
Mwenyekiti wa KRFA Jamal Malinzi  akiwa na baadhi ya wajumbe wa kamati tendaji,katika picha ya pamoja mbele ya kifaa kinachotumika kutengeneza uwanja wa kaitaba.

No comments:

Post a Comment