Saturday 20 June 2015

BAADA YA KUKUTA UMATI WA WATU UWANJA WA NDEGE BUKOBA,BERNARD MEMBE ATEMBEA KWA MGUU MPAKA OFISI ZA CHAMA.

Katika hali ambayo haikutegemewa na wengi waziri wa mambo ya nchi za nje  na mahusiano ya kimataifa Mh Bernard Membe baada ya kutua kwenye uwanja wa ndege kusaka wadhamini  mkoa wa Kagera na kukuta umati mkubwa wa watu waliokuja kumpokea uwanja wa ndege aliamu kutembea nao mpaka katika ofisi za ccm mkoa ambako shughuli ya udhamini ilikuwa ikifanyika,(Pichani ni mh Membe akitembea na wananchi kuelekea ofisi za chama,takribani km 4) Mmoja ya watu walioongozana nae katika msafara wake ambae sikupata jina lake alisema mh Membe atatembea na wananchi maana hawezi kupanda gari na wananchi waliokuja kwa wingi watembee kwa mguu,alisema ana afya njema ya kutembea au kukimbia bila matatizo.Mh Membe amedhaminiwa na zaidi ya wanachama 500.

Mh Membe akiwa na Mzee Faustin Kamaleck Katibu mstaafu ccm Mkoa wa Kagera.
Katibu wa uvccm Mkoa wa Kagera Didas Zihimbile akitoa utaratibu uwanja wa ndege Bukoba.
Mwenezi wa ccm Bkoba mjini Ramadhani Kambuga akisalimiana na mh Membe.

Mh Membe akitembea.