Monday 15 June 2015

LOWASSA MAPOKEZI YAKE BUKOBA LEO,WANASEMA MAFURIKO HAYAZUIWI NA VIGANJA,AJIZOLEA WADHAMINI RUKUKI.

Waziri mkuu mstaafu Bw Edward Lowassa amefika makao makuu ya mkoa wa Kagera, Bukoba Manispaa na kupokelewa na maelfu ya wananchi katika uwanja wa ndege wa Bukoba na kumsindikiza kwa kidedea kuelekea makao makuu ya ccm Mkoa kwa ajiri ya kupata wadhamini katika mchakato mzima wa kuomba ridhaa katika chama cha ccm kupererusha bendera ya nafasi ya uraisi mwezi wa kumi mwaka huu,Mh Lowassa ambae anaonyesha kuwa na mvuto kwa wananchi kila anapofika katika mikoa mbalimbali ,amekuwa akipokelewa na wananchi wengi sana.Kwa Bukoba watu wazima na vijana wameonekana kumuunga mkono kwa wingi,akiongea na wananchi wengi waliojitokeza kwenye ofisi za ccm mkoa mh Lowassa pamoja na kuwashukuru wananchi ameongea sababu zilizomfanya aombe nafasi ya urais,amesema umefika wakati wa kuwa na serikali yenye kutoa maamuzi na kuyatekeleza, tena maamuzi magumu,Amesema anauchukia sana umasikini, hivyo anataka watu wachape kazi na wapewe hongera ya kazi sio pole ya kazi.
Ni ndege anayotumia Mh Lowassa.
Mh Lowassa akisalimiana na Murungi kichwabuta uwanja wa ndege Bukoba.
Bw Mzee Kabaka akisalimiana na mh Lowassa.
Umati uliojitokeza kumpokea.
Katibu wa ccm Bukoba Vijijini akimkabidhi orodha ya wanachama waliomdhamini.
Mh Lowassa akiongea na wananchi.
Endelea kuangalia Jmcobukoba.blogspot .com

No comments:

Post a Comment