Friday 19 June 2015

BERNARD MEMBE KUTUA BUKOBA 20-6-2015 JUMAMOSI KUPATA WADHAMINI.

 Waziri wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa Bernard Membe atawasili Bukoba siku ya Jumamosi saa nane mchana katika uwanja wa ndege wa Bukoba kwa ajiri ya kupata wadhamini  katika harakati za kukamilisha taratibu za chama cha mapinduzi kuomba ridhaa ya kugombea nafasi ya rais,Mh Membe ni miongoni mwa makada wa ccm ambao wanatajwa kuwa na nafasi kubwa ya kupeperusha bendera ya ccm katika uchaguzi wa urais mwaka huu.Jamcobukoba.blogspot.com wakiongea na mmoja wa watu wa karibu wa Membe ,amesema wanawashukuru watanzania kwa namna ambavyo kila wanapokwenda wanajitokeza kwa wingi kumdhamini, na hii ni picha tosha kuwa Mh Membe ni chaguo la mungu na watu,akaongezea kwa kusema anawaomba wanaBukoba na Kagera kwa ujumla wajitokeze kwa wingi kumdhamini hiyo Jumamosi 20-6-2015 kuanzia uwanja wa ndege mpaka kwenye ofisi za chama.

No comments:

Post a Comment