Tuesday 28 May 2019

BW RAHIM KABYEMELA FUTURISHA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM,MKUU WA WILAYA BUKOBA AWAOMBA WADAU WENGINE KUSAIDIA.

 Bw Rahim Kabyemela Mkazi wa Manispaa ya Bukoba amefuturisha watoto wenye mahitaji maalum wa Shule ya Mugeza Viziwi,Shule Ya Msingi Mugeza Mseto yenye wanafunzi walemavu wa viungo,macho na Albino,Katika hafla hiyo mgeni rasmi Mh Mkuu wa Wilaya Bukoba Deodatus Kinawilo amewataka wadau wengine kuwa na moyo wa huruma kama  Ndugu Rahim kusaidia watoto wenye mahitaji maalum,viongozi mbalimbali wa dini,kisiasa na serikali walishiriki futari na watoto hao.