Naibu
Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajabu Luhwavi na Kaimu Katibu wa NEC, Siasa
na Uhusiano wa Kimataifa Dk Pindi Chana wameondoka Rasmi katika Utumishi
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kufuatia Rais Dk. John Magufuli kuwateua
kuwa Mabalozi watakaoiwakilisha Tanzania katika nchi za nje
watakazopangiwa baadaye.
Rais
wa Dk. Magufuli amefanya uteuzi huo leo Desemba 3, 2016, Luhwavi na Dk.
Pindi Chana wakiwa miongoni mwa Mabalozi 15 walioteuliwa ili kujaza
nafasi zilizo wazi katika Balozi za Tanzania zilizopo katika nchi
mbalimbali.
Taarifa
iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na kusambazwa na
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam, imeeleza
kuwa Mabalozi hao wameteuliwa kwa ajili ya kuiwakilisha Tanzania katika
vituo vifuatavyo;
1. Beijing - China2. Paris - Ufaransa
3. Brussels - Makao Makuu ya Jumuiya ya Nchi za Ulaya
4. Muscat - Oman
5. Rome - Italy
6. New Delh- India
7. Pretoria - Afrika ya Kusini
8. Nairobi - Kenya
9. Brasilia - Brazil
10. Maputo - Msumbiji
11. Kinshasa - Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
12. Kampala - Uganda
13. Abuja - Nigeria
14. Moroni - Comoro
15. Geneva - Umoja wa Mataifa
Aidha, Rais Magufuli amefanya uteuzi wa Mabalozi sita kwa ajili ya kuiwakilisha Tanzania katika Balozi mpya sita ambazo zitafunguliwa hivi karibuni katika nchi za Algeria, Israel, Korea ya Kusini, Sudan, Qatar na Uturuki.
Orodha kamili ya Mabalozi walioteuliwa ni kama ifuatavyo;
1. Balozi Mbelwa Brighton Kairuki
2. Balozi Samuel W. Shelukindo
3. Balozi Joseph E. Sokoine
4. Balozi Silima K. Haji
5. Balozi Abdallah Kilima
6. Balozi Baraka Luvanda
7. Balozi Dk. James Alex Msekela
8. Balozi Mteule Sylvester Mwakinyuke Ambokile
9. Balozi Mteule Dk. Pindi Chana
10. Balozi Mteule Dk. Emmanuel J. Nchimbi
11. Balozi Mteule Rajab Omari Luhwavi
12. Balozi Mteule Lut. Jenerali Mstaafu Paul Ignace Mella
13. Balozi Mteule Grace Mgovano
14. Balozi Mteule Mohamed Said Bakari
15. Balozi Mteule Job Masima
16. Balozi Mteule Omar Yusuf Mzee
17. Balozi Mteule Matilda S. Masuka
18. Balozi Mteule Fatma M. Rajab
19. Balozi Mteule Sylvester M. Mabumba
20. Balozi Mteule Prof. Elizabeth Kiondo
21. Balozi Mteule George Madafa ambaye uteuzi wake ulishatangazwa
Vituo vya kazi vya mabalozi hawa 21 vitatangazwa baadaye na Mabalozi wote waliobaki katika vituo ambavyo si kati ya vituo hivi 15 vilivyotajwa wataendelea na nafasi zao za uwakilishi wa Tanzania katika vituo walivyopo.
Katika hatua nyingine, Mhe. Rais Magufuli amemhamisha Balozi Modest Jonathan Mero kutoka kituo chake cha sasa cha Geneva, kwenda Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (New York) ambako atakuwa Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa.
Mhe. Balozi Modest Jonathan Mero anachukua nafasi ya Mhe. Balozi Tuvako M. Manongi ambaye atastaafu ifikapo tarehe 06 Desemba, 2016.
Katika hatua nyingine, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bibi Grace A. Martin kuwa Balozi na Mkurugenzi wa Itifaki (Chief of Protocal) – Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki kuanzia leo tarehe 03 Desemba, 2016.
Kabla ya uteuzi huo Bibi Grace A. Martin alikuwa akikaimu nafasi hiyo.
Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Balozi Peter Kallaghe kuwa Afisa Mwandamizi Mwelekezi – Mambo ya Nje katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi (National Defence College)
Kabla ya uteuzi huo, Balozi Peter Kallaghe alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza hadi mwanzoni mwa mwaka huu 2016.