Baada ya kutoka kanisani Bw na Bi Renatus Rutta maarufu Vijisent walipita maeneo malumu kwa ajili ya kupiga picha za pozi tofauti.
Pande za Bukoba hotel.
Endelea kufuatilia nini kilijiri ukumbini.
Tuesday, 1 November 2016
MPOKI ATEMBELEA WAHANGA WA TETEMEKO BUKOBA, AKUTANA NA MKUU WA MKOA KAGERA.
Msanii maarufu wa vichekesho nchini Tanzania wa kundi la The Comedy Bw Mpoki amemtembelea Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salumu Mstafa Kijuu ofisini kwake na kumpa pole na kazi kubwa anayoendelea nayo ya kuratibu zoezi zima la wahanga wa tetemeko la ardhi lililotokea 10-9-2016 mkoani Kagera na kusababisha athari kubwa na vifo,pia alipata nafasi ya kutembelea maeneo yaliyoathirika sana na tetemeko katika kata ya hamugembe, alitembelea kituo cha kulelea watoto yatima cha Uyacho ambacho kilibomoka chote,Bw Mpoki aliguswa sana baada ya bibi Saada kumueleza hali halisi na kumpa kiasi cha fedha kwa ajili ya kununua cementi na kuhaidi kupeleka taarifa ya uhitaji mkubwa wa msaada kwa wasanii wengine ili waje kusaidia.(katika picha Bw Mpoki akiwa na mkuu wa mkoa wa Kagera , ofisini kwake.)Mpoki akiwa na mlezi wa kituo cha watoto yatima cha Uyacho kilichopo katika kata ya Hamugembe Bukoba, kwa sasa wanalala katika jumba la mabati ambalo linajoto kubwa sana na si salama kwa afya za watoto.
Mmoja wa watoto 35 amba wapo kwa sasa katika kituo hicho.
Bibi saada akiongea kwa masikitiko.
Bw Mpoki akiwa na watoto yatima katika nyumba yao iliyobomoka .
Mpoki akiwa na washabiki wake maeneo ya Hamugembe Bukoba.
Maeneo ya hamugembe yaliyoathirika.
Mpoki akijionea maisha ya watu baada ya tetemeko.
Ndugu mwananchi kuwa na moyo wa kizalendo saidia wahanga Kagera.
Subscribe to:
Posts (Atom)