Sunday 19 July 2015

SAFARI YA BEN KATARUGA YAANZA RASMI,ARUDISHA FOMU YA UBUNGE JIMBO LA SEGEREA.

 Leo safari ya kijana mdogo kwa umri lakini mkubwa kwa hekima ,busara,uelewa,anayesimamia hoja na mtazamo wa mbele zaidi na  mpenda maendeleo Ben Kataruga amerejesha fomu za kugombea ubunge jimbo la Segerea Mkoa wa Dar es salaam  kupitia chama cha Mapinduzi. Akiongea na wanachama na baadhi ya wananchi wa jimbo la segerea Bw Ben ameseme ametambua na kuheshimu matakwa na ombi la wana segerea kugombea  ubunge,akasema anaamini  mungu kupitia kwa wana segerea kanyoosha mkono wake, na sauti ya watu ni sauti ya mungu,Bw Ben ambae ni kijana msomi ameongea kwa kujiamini na kusema umefika wakati sasa vijana kutambua wajibu wao wa kulitumikia Taifa kwa kutatua kero za wananchi na kuwaletea kile wanachokitarajia.


 Bw Ben akiwa na mmoja wa wototo yatima.

Bw Ben akiwa na watoto yatima ambao amekuwa akiwasaidia, na sasa yuko kwenye mchakato wa kuwajengea bweni la kulala.

No comments:

Post a Comment