Sunday, 19 July 2015

NI SHEREHE YA MAPOKEZI YA JOE JONATHAN NYAMWIHURA NA MKE WAKE NIURIS,HISTORIA YAO WENGI WATOA MACHOZI.

Ilikuwa ni siku ya pekee katika familia ya Jonathani Nyamwihura wa Bububa Kitobo pale alipomkaribisha mwanae Joe Jonathani Nyamwihura anaeishi nchini Cuba akiwa na mkewe na mwanae walipokaribishwa nyumbani rasmi kwa mara ya kwanza nchini Tanzania Mkoa wa Kagera Bukoba .Dr Jonathani Nyamwihura( wa kwanza kushoto) miaka 26 akiwa nchini Cuba kimasomo alimzaa Joe na mama wa kirusi ambae kwa sasa ni marehemu aliondoka nchiniCuba   na kumuacha mwanae akiwa na umri wa miaka nane, hakuwahi kukutana na mwanae kwa kipindi chote  mpaka sasa  ndio wameonana akiwa ameoa na akiwa na mtoto.Hakika ilikuwa ni furaha katika familia ya Nyamwihura. katika picha ni Dr Jonathani Nyamwihura,Joe Nyamwihura, Mjukuu,Mke wa Joe, Mama Mlezi wa Joe   Mdogo wa Joe,Familia hii yote ndio kwa mara ya kwanza wanafaamiana.Hakika ni story inayotia majonzi na furaha.


Wanafamilia ya Nyamwihura.

Dr Nyamwihura muda wote alikuwa full shangwe.
Bw Chichi.
Rafiki wa familia kutoka Uganda.
Nshomile akitumbuiza.
Kiongozi wa dini akiombea chakula.
Joe na  mkewe wakichukua chakula.
Dr Fred Ruila akichukua chakula.
Mrs Jonathan Nyamwihura akiwa na mjukuu.


Mama mzazi wa Dr Jonathan Ma Christina Nyamwihura(kushoto)
Mc akiwa na mwenyekiti wa kamati.
Keki ikakatwa.


Shangazi akapewa keki.
Bibi akapewa keki.
Mwenyekiti wa kamati akapewa keki.
Mjukuu akacheza ngoma,japo ni mara ya kwanza kuona.
Dr Nyamwihura  akitambulisha ndugu na jamaa.
Chichi akitambulisha wanafamilia.
Joe akitoa neno la shukrani.
Mjukuu nae akaongea.
Zawadi zikatolewa.
Zawadi
Machozi ya furaha.
Dr Nyamwihura alikuwa na furaha kubwa.
Umejifunza nini msomaji?

No comments:

Post a Comment