Saturday, 19 April 2014

PILIKAPILIKA ZA PASAKA BUKOBA,WAFANYABIASHARA WA VYAKULA WAUZA,UPANDE WA MAVAZI WENGI NENO HALI MBAYA LATAWALA.

 Ikiwa kesho ni sikukuu ya  Pasaka, Mwokozi  yesu kristo alieteswa na kufa msalabani kwa ajili ya mwanadamu inasherekewa duniani kote, Katika Manispaa ya Bukoba watu wengi  wameonekana barabarani wakipitapita huku na kule kwa ajili ya manunuzi na maandalizi ya Pasaka.Camera yetu ilipita maeneo mbalimbali na kujionea hali halisi, wengi wa wafanyabiashara wa vyakula wameonekana kuwa na furaha na kusema kuwa wanashukuru mungu biashara zao zimekwenda vizuri, huku wafanyabiashara wa nguo kulalamika na kusema  biashara si nzuri inaonekana ukata umetawala.
 Maeneo ya soko kuu kwa muuza viatu anasema biashara  si nzuri
 Dada Doro anasema mauzo si makubwa kama alivyotegemea
 Mama huyu anasema biashara mbaya, anawakaribisha wenye matumbo makubwa wafike kibandani kwake soko kuu wanunue mkanda wa kupunguza tumbo
 Mama Hawa Hasani akiwa katika manunuzi ya vyakula
 Watu kibao soko kuu
 Pilikapilika soko kuu
 Viungo
 Vyakula kibao
 Gozbart akifanya manunuzi
 Mama Achi na swaiba wake
 Maduka ya nguo majanga
 Mama Visram  katika hekaheka za Pasaka, mvua kubwa sana zimenyesha Asubuhi
 Ni furaha wakiwa kwenye maandalizi ya pasaka
 Dada Unice akiwa na Dada Enjoey
 Sadati akiwa dukani kwake
 Kijana Veda Mtaani
Jamcobukoba.blogspot.com tunawatakia Pasaka njema

Friday, 18 April 2014

EXCLUSIVE,MH:MWIGULU NCHEMBA AFUTA POSHO ZA WAJUMBE WALIOSUSIA BUNGE LA KATIBA,AAGIZA BENKI KUSITISHA CHEQUE ZOTE.E

MWIGULU NCHEMBA1 
Wizara ya Fedha kupitia Naibu wake Waziri wa fedha Mh. Mwigulu Nchemba wametangaza uamuzi wa kufuta malipo ya Wabunge waliosusia vikao vya mchakato wa Katiba vinavyoendelea Dodoma.
Uamuzi huu umetangazwa ikiwa ni siku ya pili tangu Wajumbe wa Bunge la Katiba Kutoka UKAWA wasusie Shughuli za Bunge la Katiba kwa Madai wamechoka matusi na Kuburuzwa kwenye Bunge hilo.
Hii leo Naibu waziri wa Fedha Mh.Mwigulu Nchemba ambaye kwa Sasa anakaimu Kuwa Waziri wa Fedha tangu April 10  20014 baada ya  Waziri wa Fedha kupata safari ya kikazi nchini Marekani,amefuta Malipo ya wabunge waliosusia Mchakato huo wa Katiba.
Mheshimiwa Mwigulu Nchemba ameagiza Benki zote kurudisha Cheque za Malipo ya Posho na seating allowance ambazo zilipelekwa Bungeni April 16 ili ziwekwe kwenye akaunti binafsi za Wabunge ikiwa ni Malipo ya Mpaka April 30. 
Bonyeza play kumsikiliza Mh.Mwigulu Nchemba akielezea hili

Mwigulu Insert 18April2014


WAUMINI WA DINI YA KIKRISTU WAHUDHURIA IBADA MAALUM YA IJUMAA KUU LEO KANISA LA KKKT


Muumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Usharika wa Azania Front, Moses Kombe, (katikati) na wenzake wakiigiza igizo la kumbukumbu ya Kuwambwa Yesu Kristo miaka 2000 iliyopita wakati wa ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika katika kanisa hilo Dar es Salaam leo.
Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowasa akiwa katika ibada ya Ijumaa Kuu katika Kanisa la KKKT la Azania Front Dar es Salaam.
Waumini wa Kanisa la Kiinjili Tanzania KKT, la Azania Front la Dar es Salaam wakiwa katika Ibada ya Ijumaa Kuu.
Waumini wa Kanisa la Mtakatifu Joseph wakiwa kwenye ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika leo kanisani hapo.
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Kanisa Katoriki,Mwadhama Porkap Kadinali Pengo akiubusu Msaraba wakati wa ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam leo.
Waumuni wa Kanisa la Mtakatif Joseph Jimbo Kuu la Dar es Salaam wakiwa wanaubusu Msaraba wakati wa ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Mtoto, Vanes Mpupua akiubusu Msaraba wakati wa ibada ya Ijumaa Kuu katika Kanisa la Mtakatif Josef Dar es Salaam.
Mmoja wa Watoto waliofika katika Kanisa la Mtakatif Josef akiubusu Msaraba wakati wa Ibada ya Ijumaa Kuu iliofanyika Dar es Salaam

JESHI LA POLISI LATAHADARISHA WANANCHI KUWA MAKINI WAKATI WA SIKUKUU YA PASAKA.


SSP ADVERA SENSO
Tunapoelekea kipindi hiki cha sikukuu ya Pasaka, Jeshi la Polisi nchini, linatoa tahadhari kwa wananchi kuwa makini katika suala la usalama wa maisha na mali zao. 

Uzoefu unaonyesha kwamba, katika kipindi kama hiki cha sikukuu kuna baadhi ya watu hupenda kutumia fursa hiyo kufanya vitendo vya uhalifu. Hata hivyo, Jeshi la Polisi katika mikoa yote limejipanga vizuri kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kuhakikisha kwamba hakuna vitendo vyovyote vya uhalifu vitakavyojitokeza na endapo vitajitokeza viweze kudhibitiwa kwa haraka. 

Aidha, ulinzi umeimarishwa kwenye maeneo yote, yakiwemo maeneo ya kuabudia, fukwe za bahari, sehemu za starehe na maeneo mengine ambayo yatakuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu. 

Vilevile, Jeshi la Polisi linawataka madereva na watu wote watakaokuwa wakitumia barabara, kuwa makini na kuzingatia sheria za usalama barabarani, kuepuka kwenda mwendo kasi, kujaza abiria kupita kiasi na kutumia vilevi wawapo kazini. 

Wamiliki wa kumbi za starehe wazingatie uhalali na matumizi ya kumbi zao katika uingizaji wa watu kulingana na uwezo wa kumbi hizo, badala ya kuendekeza tamaa ya fedha kwa kujaza watu kupita kiasi. 

Aidha, wazazi wawe makini na watoto wao, kutokuwaacha watembee peke yao ama kwenda disko toto bila kuwa chini ya uangalizi wa watu wazima ili kuepusha ajali na matukio mengine yanayoweza kusababisha madhara juu yao. 

 Wananchi wakumbuke kutokuacha makazi yao bila uangalizi na endapo italazimu kufanya hivyo watoe taarifa kwa majirani zao, na pale wanapowatilia mashaka watu wasiowafahamu wasikae kimya, watoe taarifa haraka kwenye vituo vya polisi vilivyo karibu yao, ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa haraka. 

 Mwisho, Jeshi la Polisi linapenda kuwashukuru wale wote ambao tayari wamefunga kamera za CCTV katika maeneo yao ya biashara hususani yale yanayokuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu, yakiwemo maduka, mahoteli na maeneo ya benki. 

Jeshi la Polisi linaendelea kuwasisitiza ambao bado hawajaweka kamera hizo, kuweka ili ziweze kusaidia kubaini wahalifu na hata kurahisisha ukamataji wa wahalifu hao endapo uhalifu unatokea. 

 Tunawatakia Watanzania wote Pasaka njema. 

Rais Kikwete akerwa na kitendo cha wanasiasa kumtukana Mwalimu Nyerere....Asema ni utovu wa nidhamu kuwatukana waasisi wa Tanzania

 
Rais Jakaya Kikwete amesema ni utovu wa nidhamu na ukosefu wa adabu unaoonyeshwa na baadhi ya Watanzania kuwatukana, kuwadhihaki na kuwakejeli waanzilishi wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume.
Rais Kikwete alitoa kauli hiyo juzi alipokuwa kwenye mahojiano maalumu na wahariri wa baadhi ya vyombo vya habari (wa Mwananchi hawakuwapo) ya kuadhimisha miaka 50 ya Muungano.
Kauli hiyo ilikuwa ni jibu la moja ya maswali alilokuwa ameulizwa na wahariri hao kuhusu matusi, kejeli na dhihaka ambazo zimekuwa zinaonyeshwa na wajumbe wachache wa Bunge Maalumu la Katiba juu ya waasisi hao wa Tanzania na wabunifu wakuu wa Muungano wa Tanzania.
“Ni kukosa adabu na ni utovu mkubwa wa nidhamu kwa Mtanzania yeyote kuwatukana, kuwadhihaki au kuwakejeli waasisi wa Taifa letu. Hawa ni watu ambao waliifanyia nchi yetu mambo makubwa,” alisema Rais Kikwete na kuongeza:

Wednesday, 16 April 2014

HII NDIO SARE YA UZINDUZI WA MBIO ZA MWENGE KITAIFA 2014 KWA WAKAZI WA MANISPAA YA BUKOBA

 Mwl Joyce Lobozi akimuonyesha mmoja wa wahitaji
 Muonekano wa Kitenge, kwa wanaume unashona shati la mikono mirefu, na wanawake unaweza kushona kadri upendavyo
 Mwl John Mugango akichukua Kitenge kwa ajili  ya kushona shati
 Kitenge kinapatikana kwa shilingi 12,000 tu, wasiliana na Mwalimu Joyce Lobozi
 Ma KEMI nae akiangalia kitenge
Bi Eveline Agricola ukifika Manispaa ya Bukoba kitengo cha store utamkuta na utajipatia maelezo kuhusiana na vitenge