Saturday, 12 October 2013

KAGERA SUGAR 1 v YANGA 2, KAGERA WALA KICHAPO KAITABA,PAMOJA NA KUBADILISHA VIINGILIO UWANJA WAFURIKA


Kikosi cha Kagaera Sugar kilichoanza

Kikosi cha Yanga kilichoisambaratisha kagera na kuvunja  mazoea ya miaka miwili mfululizo ya kuifunga yanga katika uwanja wa kaitaba

Waamuzi wa mtanange huu

Waamuzi na Timu Kapteni wakiteta jambo muda mfupi kabla ya mpira kuanza

Benchi la Yanga kushoto ni Kocha mkuu

Benchi la Kagera Sugar

Dakika ya 2 Mpira ukirushwa kama kona na Kipa kuupangulia kwa adui na Hatimaye Mshambuliaji wa Yanga Mrisho Ngassa akafanikiwa kuipatia bao na hapa walikuwa wanashangilia bao hilo. Mpaka Mapunziko Yanga ilikuwa inaongoza kwa bao 1-0 dhidi ya Wenyeji Kagera Sugar. Habari na www.bukobasports.com

Wachezaji wa Yanga wakishangilia Baada ya kupata bao kupitia kwa Mrisho Ngassa

Kama Kawaida Yanga wanapofunga kufurahia kwa aina hii si ajabu

Raha ya Ushindi..jamani..

Asante Ngassa

Chukua tano kwanza ....Asante!!

Patashika Uwanjani..
Baadhi ya Mashabiki waliojitokeza kwa wingi kwenye Uwanja wa Kaitaba.Pamoja na viingilio kubadilishwa dakika za mwisho kutoka 5000 jukwaa kuu na 3000 mzunguko na kuwa 10.000 jukwaa kuu na 5000 mzunguko watu wamefurika kwa wingi kushuhudia mpambano huo.
Kipindi cha pili dakika ya 49 Godfrey Wambura akaisawazishia bao timu yake na kufanya 1-1 na mtanange Kuchangamka sana kuliko kipindi cha kwanza..
Dakika ya 60 Hamis Kiiza akaiongezea bao Yanga na kufanya 2-1 Dhidi ya Wenyeji Kagera Sugar.

Friday, 11 October 2013

SHEHENA YA VIFAA VYA WABUDIO SHETANI VYAKAMATWA BANDARI YA MOMBASA



8
9
10
Kontena ambalo lilikuwa na vitu vya nyumbani, limekamatwa likiwa na bidhaa nyingi za ajabu kama mafuvu na vitu vingine vya kutisha ambavyo inasemekana huwa vinatumika kwenye ibada za dini za kishetani. Mzigo huo bado unashikiliwa na mamlaka za Kenya na hii hapa audio ya ripoti nzima pamoja na video ya mzigo wenyewe kama ilivyoripotiwa na Citizen TV

TASWIRA YA AJALI ILITOKEA MKOANI TANGA


Hii ndiyo taswira ya ajali kati ya lori na basi la abiria,ajali hii imetokea maeneo ya kabuku mkoani Tnga.

MUSTAFA HASSANALI AZINDUA VIWALO EQUATORIAL GINEA





 
"Esmeralda" was launched at Malabo international fashion Week by designer Mustafa Hassanali on 28 September. The Collection was inspired by the beauty and fluidity of the gem Emerald which depicts the richness and lushness of the chiffon's and Brocades that's drape the canvas of the Women of 21st Century.

YANGA WAKIFANYA MAZOEZI YAO LEO KWENYE UWANJA WA KAITABA KESHO KUVAANA NA WENYEJI KAGERA SUKARI


Wachezaji wa Yanga na Viongozi wao mkoni kagera wakijiandaa na mpambano na wenyeji Kagera Sugar...
Kikosi cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom timu ya Young Africans kesho kitashuka dimbani kupambana na wenyeji wakata miwa wa Kagera Sugar katika mchezo utakaofanyika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba kuanzia majira ya saa 10:00 kamili kwa saa za Afrika Mashariki.
Timu ya Young Africans iliwasili jana asubuhi mkoani Kagera kwa shirika la ndege la Precison ikiwa na kikosi cha wachezaji 21 na viongozi 10 ambapo jioni kikosi kilifanya mazoezi katika uwanja wa shule ya seminari ya Ntungamo.

Pamoja na kuwa na mvua na hali ya hewa ya baridi asubuhi mjini Bukoba, wapenzi washabiki na wanachama wa Young Africans walijitokeza kwa wingi uwanja wa Kaitaba leo asubuhi kushuhudia mazoezi ya watoto wa jangwnai yaliyokuwa yakiongozwa na kocha mkuu Ernie Brandts.
Mara baada ya mazoezi hayo, kocha Brandts amesema anashukuru vijana wake wote wapo fit, hakuna majeruhi na wanaendelea na maandalizi ya mchezo huo wa kesho dhidi ya Kagera Sugar."Kiujumla kikosi changu kipo vizuri, kama unavyoona wachezaji wana ari na morali ya hali ya juu kuelekea kwenye mchezo huo ambao kwetu ni muhimu sana kuhakikisha tunapata ushindi" alisema Brandts.
Aidha Brandts alisema anajua Kagera Sugar wana timu nzuri, na wanautumia uwanja wao wa nyumbani vizuri kupata ushindi kama msimu uliopita lakini msimu huu kikosi chake kimejipanga kuhakikisha kinapata ushindi, uwezo na nia wanayo hivyo hawaoni sababu ya kuwazuia kukosa ushindi.

Mchezo utaanza majira ya saa 10:00 kamili kwa saa za Afrika Mashariki na viingilio vya mchezo huo vitakua ni Tshs 5,000/= kwa Jukwaa Kuu na Tshs 3,000/= kwa mzunguko.
Wapenzi na washabiki wa soka mnaombwa kujitokeza kwa wingi kuja kukishangilia kikosi cha Young Africans kitakapokuwa kinapambana na wenyeji Kagera Sugar.




Kesho ni kazi ya kufa na kupona




Kazi ni kesho Jumamosi Kaitaba kutafuta pointi 3 muhimu sana...

Wachezaji wa Yanga wakiendelea na mazoezi kwenye uwanja wa Kaitaba Mjini Bukoba leo hii

Niyonzima kushoto akifanya mazoezi leo hii kwenye uwanja wa Kaitaba


RATIBA:
Jumamosi Oktoba 12
Kagera Sugar v Yanga
Simba v Tanzania Prisons

Jumapili Oktoba 13
Ashanti United v Coastal Union
Ruvu Shooting v Rhino Rangers
Mgambo JKT v Mbeya City
Azam FC v JKT Ruvu
Mtibwa Sugar v JKT Oljoro

MSIMAMO ULIVYO KWA SASA.
NA
TIMU
P
W
D
L
GD
GF
POINTI
1
Simba SC
7
4
3
0
11
16
15
2
Azam FC
8
3
5
0
5
11
14
3
Mbeya City
8
3
5
0
4
11
14
4
Yanga SC
7
3
3
1
6
13
12
5
JKT Ruvu
8
4
0
4
3
9
12
6
Coastal Union
7
2
5
0
3
6
11
7
Kagera Sugar
7
3
2
2
2
7
11
8
Ruvu Shooting
8
3
2
3
2
9
11
9
Mtibwa Sugar
8
2
4
2
-2
7
10
10
Rhino Rangers
8
1
4
3
-3
8
7
11
Prisons FC
7
1
4
2
-5
4
7
12
JKT Oljoro
8
1
3
4
-3
6
6
13
Mgambo JKT
8
1
2
5
-11
2
5
14
Ashanti United
7
0
2
5
-11
4
2