Makamu
wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata
utepe ikiwa ni ishara ya kuzindua rasmi Miradi ya
ukarabati wa Vituo vya Kupoza Umeme na Ujenzi wa Njia ya kusafirisha
Umeme katika Mkoa wa Kilimanjaro. Hafla hiyo ya uzinduzi imefanyika leo,
Oktoba 7, 2013 katika Kituo cha kupoza umeme cha Makuyuni Wilaya ya
Moshi
Vijijini Tarafa ya Himo Mkoa wa Kilimanjaro. Kutoka
kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Tanesco, Felician Mramba, Waziri wa
Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo (kushoto kwa Makamu) ni Balozi
wa Japan nchini, Masaki Okada na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas
Gama.
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifunua
kitambaa ikiwa ni ishara ya kuweka Jiwe la msingi,
katika uzinduzi rasmi Miradi ya ukarabati wa Vituo vya Kupoza Umeme na
Ujenzi wa Njia ya kusafirisha Umeme katika Mkoa wa Kilimanjaro. Hafla hiyo ya uzinduzi imefanyika leo,
Oktoba 7, 2013 katika Kituo cha kupoza umeme cha Makuyuni Wilaya ya
Moshi Vijijini Tarafa
ya Himo Mkoa wa Kilimanjaro. Kulia ni Waziri wa Nishati na Madini,
Prof. Sospeter Muhongo na nyuma yao ni Balozi wa Japan nchini, Masaki Okada
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza
maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Tanesco, Felician Mramba, wakati
alipotembelea kukagua Kituo cha kusambaza Umeme cha Kiyungi, mkoani
Kilimanjaro.
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia
moja ya mtambo wa kisasa wa kusambaza umeme uliopo
katika kituo cha Makuyuni Wilaya ya Moshi Vijijini Tarafa ya Himo Mkoa
wa Kilimanjaro, wakati alipofika kituoni hapo kuzindua rasmi
Miradi ya ukarabati wa Vituo vya Kupoza Umeme na Ujenzi wa Njia ya
kusafirisha Umeme katika Mkoa wa Kilimanjaro, leo Oktoba 7, 2013.
No comments:
Post a Comment