Leo ilikuwa ni siku ya barua duniani na
kama kawaida yangu ya kupenda kumshirikisha msikilizaji wangu nilipata
barua.Barua hii iliandikwa tarehe 29 mwezi wa 10 mwaka 1981 ina maana
mwezi huu inatimiza miaka 32.
Barua hii aliandikiwa Charles Chopa
akiwa shuleni Lindi.Wakati huo alikuwa na miaka 17 akisoma kidato cha
kwanza.Alipotoka nyumbani Dar maeneo ya kariakoo lakini nyumbani aliacha
mama mgonjwa.
Alipopata barua hii akajua sasa mama
ndio basi tena.Barua ilifika bado wiki moja kufunga shule.Siku zikaenda
hatimae akafunga shule na kurudi nyumbani.Kufika nyumbani mama alikuwa
mahututi amelazwa muhimbili na kauli imeshakata kesho yake akafariki
dunia.
Ilimuachia simanzi na toka wakati huo
hii barua imekuwa sehemu ya maisha yake akipata changamoto za maisha
anaisoma imliwaze maana ndio maneno ya mwisho mama yake alimwambia.
Nimejaribu kugeuza picha zikae sawa zimenigomea.Kusoma inabidi usome kiupande upande daah.
Nilifurahi kwa Mr.Chopa kuja kushiriki
nasi na kushare barua yake hii ambayo anasema mkewe,watoto wake watatu
wanaijua na atatitunza mpaka Mungu atakapomchukua na atawasihi watoto
wake waitunze pia.
Je wewe una barua uliyoitunza kwa muda mrefu zaidi ya hapa?kwa nini?
No comments:
Post a Comment