Mkuu wa
Masoko na Mawasiliano wa Benki ya NBC Tanzania, Mwinda Kiula Mfugale
(katikati), Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa za Kuwekeza na Wateja Wakubwa, Andrew
Massawe (kulia) na Meneja katika kitengo hicho, Dorothea Mabonye (kushoto)
wakionyesha vipeperushi kuashiria uzinduzi rasmi wa promosheni ya ‘Weka Upewe’
ya NBC ikiwa ni moja ya matukio yatakatokwenda sambamba na maadhimisho ya mwezi
wa huduma kwa wateja wa NBC. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam leo. Zawadi zote katika promosheni hiyo zitagharimu
zaidi ya shs milioni 300.
Mkuu wa
Kitengo cha Bidhaa za Kuwekeza na Wateja Wakubwa wa Benki ya NBC, Andrew
Massawe (kulia), akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa promosheni ya ‘Weka
Upewe’ ya NBC ikiwa ni moja ya matukio yatakatokwenda sambamba na maadhimisho
ya mwezi wa huduma kwa wateja wa NBC. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es
Salaam leo. Zawadi kubwa ni gari jipya aina ya Suzuki Swift tolea la mwaka 2013.
Katikati ni Mkuu wa Masoko na
Mawasiliano wa benki hiyo, Mwinda Kiula
Mfugale na kushoto ni Meneja katika kitengo hicho, Dorothea Mabonye.
Mkuu
wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya NBC Tanzania, Mwinda Kiula Mfugale
(katikati), akijibu maswali ya waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa
promosheni hiyo. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa za Kuwekeza na Wateja
Wakubwa, Andrew Massawe na Meneja katika kitengo hicho, Dorothea Mabonye.
Meneja
katika kitengo cha Bidhaa za Kuwekeza na
Wateja Wakubwa cha NBC, Dorothea Mabonye (kushoto) akitoa ufafanuzi jinsi ya
uendeshaji wa promosheni ya Weka Upewe wakati wa uzinduzi huo jijini Dar es
Salaam leo. Katikati ni Mkuu
wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya NBC Tanzania, Mwinda Kiula Mfugale na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa za Kuwekeza na Wateja
Wakubwa, Andrew Massawe.
No comments:
Post a Comment