Wachezaji wa Yanga na Viongozi wao mkoni kagera wakijiandaa na mpambano na wenyeji Kagera Sugar...
Kikosi cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom timu ya Young Africans kesho kitashuka dimbani kupambana na wenyeji wakata miwa wa Kagera Sugar katika mchezo utakaofanyika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba kuanzia majira ya saa 10:00 kamili kwa saa za Afrika Mashariki.
Timu ya Young Africans iliwasili jana asubuhi mkoani Kagera kwa shirika la ndege la Precison ikiwa na kikosi cha wachezaji 21 na viongozi 10 ambapo jioni kikosi kilifanya mazoezi katika uwanja wa shule ya seminari ya Ntungamo.
Pamoja na kuwa na mvua na hali ya hewa ya baridi asubuhi mjini Bukoba, wapenzi washabiki na wanachama wa Young Africans walijitokeza kwa wingi uwanja wa Kaitaba leo asubuhi kushuhudia mazoezi ya watoto wa jangwnai yaliyokuwa yakiongozwa na kocha mkuu Ernie Brandts.Mara baada ya mazoezi hayo, kocha Brandts amesema anashukuru vijana wake wote wapo fit, hakuna majeruhi na wanaendelea na maandalizi ya mchezo huo wa kesho dhidi ya Kagera Sugar."Kiujumla kikosi changu kipo vizuri, kama unavyoona wachezaji wana ari na morali ya hali ya juu kuelekea kwenye mchezo huo ambao kwetu ni muhimu sana kuhakikisha tunapata ushindi" alisema Brandts.
Aidha Brandts alisema anajua Kagera Sugar wana timu nzuri, na wanautumia uwanja wao wa nyumbani vizuri kupata ushindi kama msimu uliopita lakini msimu huu kikosi chake kimejipanga kuhakikisha kinapata ushindi, uwezo na nia wanayo hivyo hawaoni sababu ya kuwazuia kukosa ushindi.
Mchezo utaanza majira ya saa 10:00 kamili kwa saa za Afrika Mashariki na viingilio vya mchezo huo vitakua ni Tshs 5,000/= kwa Jukwaa Kuu na Tshs 3,000/= kwa mzunguko.
Wapenzi na washabiki wa soka mnaombwa kujitokeza kwa wingi kuja kukishangilia kikosi cha Young Africans kitakapokuwa kinapambana na wenyeji Kagera Sugar.
Kesho ni kazi ya kufa na kupona
Kazi ni kesho Jumamosi Kaitaba kutafuta pointi 3 muhimu sana...
Wachezaji wa Yanga wakiendelea na mazoezi kwenye uwanja wa Kaitaba Mjini Bukoba leo hii
Niyonzima kushoto akifanya mazoezi leo hii kwenye uwanja wa Kaitaba
RATIBA:
Jumamosi Oktoba 12
Kagera Sugar v Yanga
Simba v Tanzania Prisons
Jumapili Oktoba 13
Ashanti United v Coastal Union
Ruvu Shooting v Rhino Rangers
Mgambo JKT v Mbeya City
Azam FC v JKT Ruvu
Mtibwa Sugar v JKT Oljoro
Simba v Tanzania Prisons
Jumapili Oktoba 13
Ashanti United v Coastal Union
Ruvu Shooting v Rhino Rangers
Mgambo JKT v Mbeya City
Azam FC v JKT Ruvu
Mtibwa Sugar v JKT Oljoro
MSIMAMO ULIVYO KWA SASA.
NA
|
TIMU
|
P
|
W
|
D
|
L
|
GD
|
GF
|
POINTI
|
1
|
Simba SC
|
7
|
4
|
3
|
0
|
11
|
16
|
15
|
2
|
Azam FC
|
8
|
3
|
5
|
0
|
5
|
11
|
14
|
3
|
Mbeya City
|
8
|
3
|
5
|
0
|
4
|
11
|
14
|
4
|
Yanga SC
|
7
|
3
|
3
|
1
|
6
|
13
|
12
|
5
|
JKT Ruvu
|
8
|
4
|
0
|
4
|
3
|
9
|
12
|
6
|
Coastal Union
|
7
|
2
|
5
|
0
|
3
|
6
|
11
|
7
|
Kagera Sugar
|
7
|
3
|
2
|
2
|
2
|
7
|
11
|
8
|
Ruvu Shooting
|
8
|
3
|
2
|
3
|
2
|
9
|
11
|
9
|
Mtibwa Sugar
|
8
|
2
|
4
|
2
|
-2
|
7
|
10
|
10
|
Rhino Rangers
|
8
|
1
|
4
|
3
|
-3
|
8
|
7
|
11
|
Prisons FC
|
7
|
1
|
4
|
2
|
-5
|
4
|
7
|
12
|
JKT Oljoro
|
8
|
1
|
3
|
4
|
-3
|
6
|
6
|
13
|
Mgambo JKT
|
8
|
1
|
2
|
5
|
-11
|
2
|
5
|
14
|
Ashanti United
|
7
|
0
|
2
|
5
|
-11
|
4
|
2
|
No comments:
Post a Comment