Sunday 18 September 2016

UVCCM TAIFA WATOA MSAADA WA CEMENTI NA WACHANGIA DAMU KWA WAHANGA WA TETEMEKO KAGERA

 Katibu mkuu wa UVCCM TAIFA Bw Shaka  Amudu Shaka na baadhi   viongozi waandamizi wa uvccm Taifa wamefika mkoani kagera kwa ajili ya kutoa mkono wa pole kwa wahanga wa tetemeko la ardhi lilotokea 10-9-2016, Bw Shaka mapema alifika ofisi ya chama mkoa na kupewa taarifa ya maafa na badae kwenda ofisi ya mkuu wa mkoa kagera kukabidhi msaada wa mifuko mia moja ya cement na baadae kuelekea uwanja wa uhuru Mashujaa Uswahilini Bukoba kwa ajili ya kutoa damu ili iweze kusaidia majerui wanaohitaji damu.(katika picha Kushoto Katibu mkuu uvccm Taifa Shaka Amudu Shaka akikabidhi cement mifuko mia moja kwa Meja Jenerali mstaafu Salumu Kijuu)
 Kushoto Katibu Mkuu Uvccm Taifa Bw Shaka akiwa na mwenyekiti wa uvccm mkoa wa Kagera Yahya Kateme.
 Zoezi la utoaji damu.
 Kushoto Waziri Mwigulu Nchemba na waziri Jenesta Muhagama wakiwasili ofisi ya mkuu wa mkoa Kagera.
 Katibu Uvccm Mkoa wa kagera Didasi Zihimbile akitoa maelezo.
 Mwenyekiti wa mkoa uvccm Kagera Yahya Kateme akitoa maelezo kwa niaba ya vijana mkoa wa kagera kuhusiana na mwenendo mzima  wa hutoaji huduma kwa wahanga.
 Katibu MKUU UVCCM TAIFA akiongea.
 Hizi ndizo namba zinazotumika kutoa msaada kwa wahanga, toa hata shilingi mia tu kusaidia.

JOKATE (KIDOTI)ATEMBELEA KITUO CHA YATIMA UYACHO,KILICHOHARIBIWA NA TETEMEKO LA ARDHI, ATOA MAGODORO.

 Mwanamitindo Jokate Kidoti ametembelea kituo cha watoto yatima cha Uyacho kilichoko kata ya Hamugembe Manispaa ya Bukoba na kuwapa pole kwa majengo yao kuanguka kwa ajili ya tetemeko la ardhi la 10-9-2016 mkoani Kagera.Jokate amewafariji yatima hao na kuwapa msaada wa magodoro,watoto hao zaidi ya arobaini kwa sasa wanaishi kwenye hema lillotengenezwa na maturubai.(katika picha Jokate akimsalimia Bibi Sada ambae ndio mlezi na mwazilishi wa kituo hicho.)
 Kushoto ni mwenyeji wa Jokate Jamal Kalumuna akiwa Jokate walipotembelea  kituo cha watoto yatima Uyacho katika kata ya Hamugembe Bukoba.
 Kulia ni katibu wa kituo.
 Watoto wakifurahia msaada wa magodoro.
 Bibi saada mlezi wa kituo akifurahi .
 Jokate akijionea hali halisi ya majengo.
 Mtangazaji wa Clouds Tv Siza akifanya mahojiano.
 Wananchi wa hamugembe wakielezea maafa waliyoyapata.
 Watu wakifurahia kitendo cha kiutu na ubinadamu alichofanya Jokate.