Sunday 18 September 2016

JOKATE (KIDOTI)ATEMBELEA KITUO CHA YATIMA UYACHO,KILICHOHARIBIWA NA TETEMEKO LA ARDHI, ATOA MAGODORO.

 Mwanamitindo Jokate Kidoti ametembelea kituo cha watoto yatima cha Uyacho kilichoko kata ya Hamugembe Manispaa ya Bukoba na kuwapa pole kwa majengo yao kuanguka kwa ajili ya tetemeko la ardhi la 10-9-2016 mkoani Kagera.Jokate amewafariji yatima hao na kuwapa msaada wa magodoro,watoto hao zaidi ya arobaini kwa sasa wanaishi kwenye hema lillotengenezwa na maturubai.(katika picha Jokate akimsalimia Bibi Sada ambae ndio mlezi na mwazilishi wa kituo hicho.)
 Kushoto ni mwenyeji wa Jokate Jamal Kalumuna akiwa Jokate walipotembelea  kituo cha watoto yatima Uyacho katika kata ya Hamugembe Bukoba.
 Kulia ni katibu wa kituo.
 Watoto wakifurahia msaada wa magodoro.
 Bibi saada mlezi wa kituo akifurahi .
 Jokate akijionea hali halisi ya majengo.
 Mtangazaji wa Clouds Tv Siza akifanya mahojiano.
 Wananchi wa hamugembe wakielezea maafa waliyoyapata.
 Watu wakifurahia kitendo cha kiutu na ubinadamu alichofanya Jokate.


No comments:

Post a Comment