Saturday 12 December 2015

PUNGUZO LA BEI KWA AJILI YA X-MAS NA MWAKA MPYA, KARIBU KWA MAMA VYOMBO SHOP MTAA WA MIGEYO BUKOBA

 Kwa mahitaji ya vyombo vyenye ubora wa hali ya juu, Mama vyombo shop walioko mtaa wa Migeyo karibu na Tawi la Benki ya  wakulimina (KFCB) Wameleta vyombo vya kila aina kwa ajili ya x-mas na mwaka mpya, katika  hali ya kujari wateja wake lipo punguzo la asilimia 20,Usiangaike kutafuta vyombo vya ubora fika mtaa wa Migeyo utajipatia kila aina ya chombo kwa bei nzuri.
 UTAJIPATIA VITI, SUFURIA KAMA UNAVYOONA.
 CHUPA ZA CHAI ZA KIWANGO.
KARIBU SANA.

Saturday, December 12, 2015 Rais Magufuli Awaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri Ikulu Dar es Salaam



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Mhongo katika hafla fupi ya kuwaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri, leo katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii na Jinsia, wazee na watoto, Ummy Mwalimu katika hafla fupi ya kuwaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri , leo katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha waziri wa Katiba na Sheria, Harrison Mwakyembe katika hafla fupi ya kuwaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri, leo katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha Naibu waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.Ashantu Kijaji katika hafla fupi ya kuwaapisha Mawaziri, leo katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha  Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Lameck Nchemba katika hafla fupi ya kuwaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri, leo katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimwapisha waziri wa Sera, Bunge, Kazi ,Vijana,Ajira na Walemavu, Dkt. Abdallah Possi katika hafla fupi ya kuwaapisha Mawaziri, na manaibu Waziri leo katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.

Wednesday 9 December 2015

NI UHURU NA KAZI,NDIVYO ILIVYOSHEREKEWA,KWA MFANYABIASHARA ALIEJENGA KWENYE CHANZO CHA MAJI MTO KANONI BUKOBA.

 Yale mazoea na ukiukaji wa sheria na kuupuza mamlaka zilizopo na kuchangiwa na watendaji wobovu na wala rushwa yamemkuta mfanyabiashara anaejulikana kwa jina la Charles White aliejenga kwenye chanzo cha maji kwenye eneo la mto Kanoni kukutana na gharika la Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba kuamuru ofisi yake kubomoa jengo hilo ,akiwa anatekeleza zoezi la kuvunja nyumba zote zilizojengwa kwenye vyanzo vya maji katika Manispaa ya Bukoba.
 Yapo maswali mengi sana ya kujiuliza, hivi huyu mfanyabiashara mpaka jengo hili linasimama nani alitoa kibali, je kama hakupewa siku zote walikuwa wapi, je kama alipewa kibali nani kawajibishwa, kama hajawajibishwa wanasubiri nini, ni maswali mengi tu ya kujiuliza, lakini hii ni awamu ya tano alisababisha na aliefanya wote wanahusika kuwajibishwa, tumeona upande mmoja tunasubiri upande wa pili.
 Wananchi wakiwa wamesimama daraja la mto kanoni barabara ya Hamugembe  wakishuhudia tukio la kubomoa nyumba.
 Mwandishi wa Star Tv Bi Mariam akiwajibika.
 Mwandishi wa TBC Charles Mwibea akiwa kwenye tukio.
 Mwandishi wa ITV Audax Mtiganzi akiwa kazini.
 Eneo hili kabla ya ujenzi lilikuwa likitumia kwa ajili ya kuandaa miche ya miti.
 Waandishi wa habari wakiojiana na mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba.
 Mkurugenzi akiongea na waandishi.
Na usafi ukiendelea, Uhuru na Kazi, Hapa ni kazi tu.

BUKOBA WAITIKIA KWA WINGI KATIKA KUSAFISHA MAZINGIRA.

 Ule msemo wa Uhuru  na kazi umetimia leo kwa vitendo, katika kutekeleza agizo la rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli kusherekea sherehe ya Uhu ru kwa kufanya kazi,Kila kona ya Manispaa ya Bukoba wananchi walionekana wakifanya usafi.(katika picha ni afisa wa Jeshi la polisi akifanya usafi eneo la Kituo cha polisi Bukoba).
 Eneo la soko kuu Bukoba
 Bw Mushamu nae akiendelea na usafi.


 Mafisa wa shirika la nyumba Bukoba nao walishiriki katika Uhuru na kazi.
 Mkuu wa wilaya ya Bukoba Jakson Msomi akimsisitiza jambo mganga mkuu wa Mkoa Kagera