Wednesday 9 December 2015

NI UHURU NA KAZI,NDIVYO ILIVYOSHEREKEWA,KWA MFANYABIASHARA ALIEJENGA KWENYE CHANZO CHA MAJI MTO KANONI BUKOBA.

 Yale mazoea na ukiukaji wa sheria na kuupuza mamlaka zilizopo na kuchangiwa na watendaji wobovu na wala rushwa yamemkuta mfanyabiashara anaejulikana kwa jina la Charles White aliejenga kwenye chanzo cha maji kwenye eneo la mto Kanoni kukutana na gharika la Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba kuamuru ofisi yake kubomoa jengo hilo ,akiwa anatekeleza zoezi la kuvunja nyumba zote zilizojengwa kwenye vyanzo vya maji katika Manispaa ya Bukoba.
 Yapo maswali mengi sana ya kujiuliza, hivi huyu mfanyabiashara mpaka jengo hili linasimama nani alitoa kibali, je kama hakupewa siku zote walikuwa wapi, je kama alipewa kibali nani kawajibishwa, kama hajawajibishwa wanasubiri nini, ni maswali mengi tu ya kujiuliza, lakini hii ni awamu ya tano alisababisha na aliefanya wote wanahusika kuwajibishwa, tumeona upande mmoja tunasubiri upande wa pili.
 Wananchi wakiwa wamesimama daraja la mto kanoni barabara ya Hamugembe  wakishuhudia tukio la kubomoa nyumba.
 Mwandishi wa Star Tv Bi Mariam akiwajibika.
 Mwandishi wa TBC Charles Mwibea akiwa kwenye tukio.
 Mwandishi wa ITV Audax Mtiganzi akiwa kazini.
 Eneo hili kabla ya ujenzi lilikuwa likitumia kwa ajili ya kuandaa miche ya miti.
 Waandishi wa habari wakiojiana na mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba.
 Mkurugenzi akiongea na waandishi.
Na usafi ukiendelea, Uhuru na Kazi, Hapa ni kazi tu.

No comments:

Post a Comment