Friday 6 December 2013

MATUKIO MBALIMBALI YA PICHA KATIKA MAZISHI YA MAREHEMU HATIFU GALIATANO YALIYOFANYIKA LEO BUGANGUZI

 Ilikuwa ni majonzi makubwa leo majira ya saa nane mchana wakati mwili wa marehemu Hatifu Galiatano ulipowasili nyumbani kwa mzee Abbakari Galiatano Buganguzi
 Tukiwa maeneo ya Buganguzi centre  tukimpa company blogger Mc Mbaraka ambae kafiwa na mjomba wake
                                Mnec wa Wilaya ya Misenye Mh Baliagati akiwasili eneo la msiba



                                                              Bw Taimul akipata chakula
                                           Abdul Galiatano na jirani akipata chakula
                                           pilau na hasa ya kwenye sinia si mchezo
  Murungi kichwabuta alikuwa  na kazi ya kuhakikisha kila aliefika msibani anapata chakula

                              Majonzi mwili ukiwasili kutokea Dar mauti yalipomkuta
                                           Shekhe Mustaph Swadick akiwasili msibani
                                                                      kisomo kikisomwa
                                     kulia ni jirani Mary Lwabizi nae alikuwepo msibani
                Kaimu shekhe wa mkoa kagera  Haruna Kichwabuta akitoa mawaidha kabla ya mazishi
                    Safari ya mwisho ya marehemu Hatifu Gariatano akiswaliwa tayari kwa mazishi

HATARIII...!Watuhumiwa wa mauaji ya Dk. Mvungi watishiana kutoana Roho Mahabusu..!!


WASHITAKIWA 10 wanaodaiwa kumwua aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk Sengodo Mvungi wameiomba Mahakama iwatenganishe rumande kwa kuwa wanapigana na kutishana kuuana.

Walidai hayo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kesi hiyo ilipotajwa mbele ya Hakimu Mkazi Sundi Fimbo. Washitakiwa hao waliiomba Mahakama iingilie kati suala lao kwa kuwa wakiwa rumande wamekuwa wanatishana kuwa watauana jambo ambalo ni hatari.

Hata hivyo, Hakimu Fimbo aliamua waendelee kukaa huko mahabusu na waelewane na kama jambo lolote litatokea watapewa taarifa na Mkuu wa Gereza.

Washitakiwa hao walidai kuwa hawajuani na wapo gereza moja, lakini wanatishiana kuuana na wameshapeleka malalamiko yao kwa Mkuu wa Gereza lakini hajachukua hatua na kuiomba Serikali ifanye uchunguzi ili ijue aliyefanya mauaji hayo.

“Serikali ikifanya uchunguzi haki itatendeka kabla ya wao kuuana wakiwa mahabusu,” alidai mmoja wa washitakiwa hao huku akionesha majeraha aliyopata mwenzake kutokana na kupigana.
Wakili wa Serikali, Yasinta Peter, alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na kuomba tarehe nyingine ya kutajwa, Hakimu Fimbo aliamua kesi hiyo itajwe tena Desemba 19.

Washitakiwa katika kesi hiyo ni Chibago Magozi (32) , John Mayunga (56), Juma Kangungu (29), aliyekuwa mlinzi wa marehemu Dk Mvungi, Longishu Losingo (29), Masunga Makenza (40), Paulo Mdonondo (30), Mianda Mlewa (40), Zacharia Msese (33), Msungwa Matonya (30) na Ahmad Kitabu (30).
Wanadaiwa kuwa Novemba 3 katika eneo la Msakuzi Kiswegere, Kibamba Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, washitakiwa hao kwa pamoja walimwua Dk Mvungi kwa kukusudia.

ANGALIA PICHA MBALIMBALI ZINAZOONYESHA MATUKIO KUHUSU MSIBA WA NELSON MANDELA



angalia watu afrika kusini walivyo na majonzi...........tizama picha hapa chini

Thursday 5 December 2013

RAIS KIKWETE AOMBOLEZA KIFO CHA MZEE MANDELA, ATANGAZA SIKU 3 ZA MAOMBOLEZO KITAIFA, BENDERA KUPEPEA NUSU MLINGOTI





Rais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za rambirambi Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini  na kupitia kwake, kwa mkewe Bi. Graca Machel, wanafamilia wote na wananchi wote wa Afrika ya Kusini kufuatia kifo cha Mzee Nelson Mandela kilichotokea  tarehe 5 Desemba, 2013 baada ya kuugua kwa muda mrefu.


Rais ameuelezea msiba huu kuwa ni msiba mkubwa kwetu sote.
"Afrika ya Kusini, Afrika na dunia kwa ujumla imepoteza mtu mashuhuri na shujaa mkubwa wa Karne ya 20 na 21.Tunaelewa  machungu waliyonayo wananchi wa Afrika ya Kusini kwa kupoteza kiongozi shupavu, jasiri, mwana mapinduzi , mvumilivu na mstahimilivu".
Ameongeza Rais Kikwete.

Rais amemuelezea  Mzee Mandela kuwa ni  kielelezo cha aina yake kwa wanadamu kwa moyo wake wa kusamehe, huruma na upendo uliomuwezesha  kuwaunganisha wananchi wa Afrika ya Kusini kuwa  taifa moja baada ya kipindi kirefu cha mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi.

"Mandela  ni mfano bora kwa wanadamu wa  jinsi binadamu muungwana anavyopaswa kuwa . Ni wajibu wa wana Afrika Kusini, Afrika na dunia kwa jumla kuiga mfano wake hasa moyo wake wa uzalendo, kujitolea hata maisha yake kwa ajili yake na wananchi wenzake" .Rais ameongeza kusema, "Tuzidi kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu Mzee Mandela  mahali pema peponi".





Kufuatia kifo hicho Rais ametangaza siku 3 za maombolezo kuanzia leo tarehe 6 hadi 8 Disemba, 2013.

Aidha, Mheshimiwa Rais ameagiza  kuwa katika siku hizo 3 bendera zote zipepee  nusu mlingoti.

Mwisho.



Imetolewa na;


Premi Kibanga,

Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,

Ikulu,

DAR AS SALAAM.


06 Desemba,2013


BREAKING NEWS... NELSON MANDELA AAGA DUNIA

 
Rais wa zamani wa Afrika Kusini ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 95 . Habari zaidi zitakujia.

AHUKUMIWA MIAKA 10 JELA KWA KUFANYA MAPENZI NA MBUZI HUKO KENYA.


Katana Kitsao
Jamaa mmoja mwenye umri wa miaka 28 amehukumiwa kwenda jela miaka kumi mara baada ya kukutwa na hatia ya kufanya tendo la ngono na mbuzi.
Katana Kitsao Gona toka Malindi nchini Kenya wiki iliyopita alikiri kufanya ngono na mnyama. 
Shuka chini kuangalia Video hiyo..... Mbuzi huyo wa kike kwa utulivu alikuwa pembeni ya chumba cha mahakama wakati hukumu hiyo ilipokuwa inatolewa. Jamaa huyo alikamwatwa mnamo tarehe 25 Novemba mara baada ya mkazi mmoja wa eneo hilo kumbamba akiwa uchi wa mnyama akimla uroda mbuzi huyo ambaye alikuwa amefungwa kamba, hii ni kwa mujibu wa The Star.
Ze Mbuzi
Mmiliki wa mbuzi huyo alifahamishwa na kufika eneo la tukio akiwa na majirani wengine ambao pia walimshuhudia Gona akiwa anafanya ngono na mnyama.
Jamaa alikamatwa na polisi na vipimo vya hospitali vinakaonyesha kweli kwamba tukio la ngono lilifanyika.
Gona aliomba msamaha kwa mahakama kwa kujitetea kuwa mke wake ni mlemavu na anamtegemea yeye ila mahakama ikajibu kuwa kosa hilo ni kubwa na akapewa siku 14 za kukata rufaa.

Wednesday 4 December 2013

BALOZI MPYA WA TANZANIA NCHINI NIGERIA DANIEL OLE NJOOLAY AMUAGA MAKAMU WA RAIS DK. BILAL


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na kumkaribisha Balozi mpya wa Tanzania  nchini Nigeri, Daniel Ole Njolay, wakati balozi huyo alipofika ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo mchana kwa ajili ya kumuaga kabla ya kuondoka nchini kwenda kuanza kazi.
Wakiwa na mazungumzo