Saturday 17 January 2015

ALIEKUWA MENEJA WA NMB BUKOBA ARBOGAST .J. MUSHOBOZI ASTAAFU UTUMISHI WA UMMA,AAGWA BUKOBA.

 Mchungaji akiwa ametokelezea.
 Ni dada mwenye mvuto na mnato anapatikana NMB Bukoba akikaribisha wageni mlangoni.
 Upande wa vinywaji walijipanga.
 Kushoto, ni dada shida katika pozz.
 Mzee na mama wakiwa wametokelezea.
 Baba na mama, Hapana chezea.
 Wadau wa NMB.
 Wadau
 Mama Muhazi na mwanae katika pozz.
 Pendeza sana my boss.
 Jamco na Bw Matovero.
 Wakiingia ukumbini.
 Mwenyekiti akifungua sherehe.
 Meneja mgeni Bw Victorine kimario akisalimia wageni.
Tutaendelea kuwaletea matukio mengine.

HALI SI SHWARI MANISPAA YA BUKOBA,PAMBANA KAMANDA MWAIBAMBE,MAJAMBAZI WASIJITAWALE.

Huyu Dada anahishi nje ya nchi katuma ujumbe huu,Tukio hili limetokea saa saba ya usiku maeneo ya Kibeta usiku wa kuamkia tarehe 17-1-2015.JINA LA HUYU DADA NI JULIA  ANETH MBAKILAKI.Leo usiku kwanzia saa 7 hapo katika Kijiji cha Magoti. Wezi wa 3 wanaume waliluka ukuta nakuingia kwa Mrs Zeulia Rweikiza wakavunja mlango wa nyumba ya uani na kumvamia binti yake Peace Rweikiza wakampiga kweli wakataka kumkata na panga, wakidai funguo za gari na kadi yake. Akawaambia gari iliisha haribika ni nzee iko stoa, alipokataa wakampiga kweli. Wapi dola?Wakamvamia mtoto wake mjukuu wakampiga naye wakamwambia lala chini wakawavuluta chumba cha pili kwa bibi mzee Ma Kostansia, wakasema tupe pesa na simu. Mkae hapa mama yuko wapi msipige kelele.

Wakati wote huo Peace akipiga kelele MSAADA waåpi, basi wakaendelea kupiga mlango nyumba kubwa nakutaka kuufungua ukakataa nyumba alalako Mrs Zeulia. Hapo ndipo Mrs Zeulia alisikia nakuogopa akakimbilia kufungua mlango wa mbele nakukimbilia mbele akiomba, mzaada akipiga mayowe kwa nguvu. Walimpomsikia walikuja kasi nakumkuta akikalibia karibu na barabara, wakampiga ngwala wakampiga saana, akaambiwa urudi utupe dora au pesa, akawaaambia pesa sina wakaendelea kumpiga akaanguta tena wakambuluza toka barabarani mpaka ndani wakamwambia utupe pesa, simu iko wapi akawapa,wakampiga tena wakaingilia masunduku wakavuruga kweli wakaanza kupakia mafuta, sabuni baadhi ya vitu dawa,nk mwisho wakapata pesa zake alikozificha wakazichukua wakamwacha hoi. Hakuna jirani,hakuna polisi nawalipofika polisi wanae wakiume wakaambiwa waje wenyewe wala hawakwenda kuona jinsi ali ilivyo. Baadaye walirudi nakuwapeleka polisi na hospitali.

Jamani mbona hakuna usalama nchi yetu hata ushirikiano wapi watu wameogopa kweli baada ya mauwaji yaliyotokea Bukoba mwisho wa mwaka jana?
Vipi waandishi wa habari hebu toeni historia kama hii kamili ili watu waone hali inapoelekea. Mrs Zeulia kaumizwa kweli kalazwa hospitali Bukoba GVT hospital.Mwende mkamwone atawapa maelezo
Mimi ni mwanae Victoria Rweikiza nilikuwa Bukoba mwezi wa desemba wakati mauaji yalipokuwa yanaendelea inaogopesha kweli.

MABASI YA PRINCES MURO YAANZA SAFARI ZA BUKOBA- DAR NA DAR- BUKOBA LEO 17-1-2015.

 Ni mabasi ya Princes Muro ambayo yameanza rasmi safari zake za Bukoba - Dar na Dar- Bukoba kuanzia 17-1-2015. Ni mabasi  mapya ya kisasa yenye vitu vingi vya kumfanya abiria afurahie  safari bila kuchoka,Viti vya vizuri  na nafasi kubwa unapokuwa umekaa,Full kiyoyozi, huku ukiangalia tv kama kwenye ndege, ukitaka kiti kilale au kurekebisha kadri unavyojisikia, wakati wa safari unapata kinywa na kitafunwa ili ufurahie safari, hakuna kurundika mizigo au kuzidisha watu kwenye siti, hakika Princes Muro ni kiboko.ofisi zao zipo stand kuu ya Mbasi Bukoba au piga simu 0655-301155. Karibuni.

 Kama kwenye ndege vileeeee..
 Kwa ndani.
 Full kiyoyozi na muziki wa taratibu.
 Bw Jalia Mgwao wakala wa mabasi haya kwa Bukoba.
 Mambo ya Digital.
 Kwa maelezo zaidi wasiliana na Jalia Mgwao kwa simu namba  0655-301155.
 Mkurugenzi wa kampuni ya utalii ya Kiroyera Tours Mary Kalikawe akiangalia mandhari ya mabasi kwa ndani.
 Aliongelea furaha yake Mkurugenzi wa Kiroyera Tours Mary Kalikawe , alisema usafiri ni kitu muhimu sana katika kukuza utalii nchini na duniani, hivyo Bukoba inapopata vitu vizuri na vya kisasa inasaidia kukuza utalii na kipato cha Mkoa wa Kagera.
 Kitu Tv wakati wote wa safari.
 Kitu New.
 Blogger Jamco akiwa na Jalia.
Ni mabasi mapya,ndio kwanza yanafunguliwa karatasi zake yakianzia rasmi safari zake Bukoba Dar leo 17-1-2015, karibuni sana, kwa maelezo zaidi piga simu ya mkononi namba 0655- 301155.