Wednesday 14 January 2015

HONGERA JAMAL MALINZI,KAITABA STADIUM UMEITENDEA HAKI.


 Nakumbuka mapema mwaka jana katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa Wa Kagera,mara baada ya kuwasili akitokea jijini Dar Mwenyekiti wa chama cha mpira Kagera  KRFA Jamal Malinzi baada ya kuchaguliwa kuwa  rais wa chama cha mpira nchini TFF alitamka kuwa uwanja wa Kaitaba utawekewa nyasi bandia na kujengwa jukwaa kubwa moja,Wengi wa wapenzi wa soka Mkoa wa Kagera walipokea kauli hiyo kwa shangwe na furaha kubwa,lakini baadhi yao walizani ni ahadi hewa walizozoea kuhaidiwa na hazitekeleziki, Kwa Jamal Malinzi imekuwa tofauti amehaidi na sasa utekelezaji umeanza,Jamcoblog tumetembelea uwanja wa kaitaba na kukuta kazi ikiendelea kwa kasi ya kuridhisha,Uwanja  huu wa kaitaba unaofadhiliwa na FIFA kwa asilimia mia moja tunaamini utakapokuwa umekamilika kwa kuwekewa nyasi bandia utakuwa umeuweka mkoa wetu  katika ramani ya dunia ya kuwa na viwanja bora nchini na kuweza kuleta mechi kubwa kuifanya Bukoba kujulikana na kuongeza wageni au utalii na kipato cha wananchi kukua na uchumi wa Mkoa kwa ujumla, Hongera Jamal Malinzi Hatukukosea kukuchagua.
 Hiyo ndio hali halisi matengenezo yakiendelea.

 Blogger wa Jamcoblog katika harakati za kuchukua  matukio.
 Mtaalamu kutoka FIFA akiwa kazini.

 Unaona, Kaitaba hiyo nyasi bandia zajaaaa.
 Mtaalamu kutoka FIFA katika harakati za kikazi.
Narudia maneno ya kihaya ( Eofisi etainamu wawe Ebaekomile) Asante Jamal Malinzi tunajivunia uwepo wako.

No comments:

Post a Comment