Wednesday 11 November 2015

CAMERA YETU MTAANI,BUKOBA

 Ni muonekano wa NMB Bukoba baada ya kufanya ukarabati wa ndani na nje.
 Duka la nguo la Gsmart.
 Mmiliki wa Gsmart, wauzaji wa nguo za kisasa za kiume na kike, viatu,urembo nk.
 Kituo cha kuuza mafuta yasiochakachuriwa, yenye ubora na viwango vinavyotakiwa,kipo Jamhuri road mkabala na jengo la NMB Bukoba.
 Duka la nguo za kiume, kike na watoto, lipo barabara ya Hindu hospital, Khadija Fashion.
 Jengo la wakaguzi wa mahesabu vyama vya ushirika linaendelea kukarabatiwa, mkabala na  kituo cha polisi Bukoba.
 Waandishi wa habari wakiyasaka matukio mtaani .
 Kataba inazidi kumeremeta.
Kaitaba kama ulaya.

NEW COFFEE TREE HOTEL YAFUNGWA KUTOA HUDUMA,BUKOBA.

 Tukiwa mtaani na camera yetu ghafla maeneo ya New Coffee Tree tumekuta magari ya kipakia vifaa mbalimbali Tv, vyombo, mashuka, Taulo ,Friji za vyumbani na vifaa vingine vilivyokuwa vikitumika hotelini, Hali hiyo ilibidi kufika na kutaka kujua kwa undani kulikoni kilichotokea,Mpiga picha hizi  alipata fursa ya kuongea na kijana mmoja aliekuwa msimamizi wa hotel hiyo ambae alikuwa mgumu kutaja jina lake alisema... Imebidi tufunge mizigo yetu baada ya Tajiri yetu kushindwa kuelewana na uongozi mpya wa chama cha ushirika wilaya ya Karagwe (KDCU) wamiliki wa hotel, ambao umechukua madaaraka hivi karibuni,ila inavyoelekea miongoni mwa wakurugenzi yupo mtu anapataka, Ila kazi wanayo maana vitu vyetu vyote tunavitoa vitajaa gari mbili zilizopo hapa... Mwisho wa kunukuu. New Coffee Tree ni moja ya hotel iliyokuwa ikitoa huduma ya malazi, chakula na vinywaji,pia huduma ya ukumbi kwa ajili ya maharusi na mikutano, Tupo kwenye jitihada za kumpata aliekuwa  amekodi hotel hii kibiashara Bw Mushema anaeishi jijini Mwanza kupata ukweli wa jambo hili.
 Eneo la jiko la nje kweupe.
 Friji zikiwa zimetolewa nje ya vyumba.

Monday 9 November 2015

KITCHEN PARTY YA OLIVIA.T. KAIZA YAFANA KATIKA UKUMBI WA LINA'S BUKOBA.

 Kulia ni Bi harusi mtarajiwa anaetegemea kufunga pingu za maisha hivi karibuni  Bi Olivia .T. Kaiza akiwa na mama yake mzazi  Bibi Gozibeltha Evalista (Mama Stella) wakiwa  katika ukumbi wa Lina's, Wa mama Bukoba walimiminika wakiwa memependeza  na kumeremeta kwa ajiri ya kumfunda na kumtakia maisha mema ya ndoa, nasaha mbalimbali zilitolewa na wamama.
 Mama mzaa chema (kulia ) Mama Stella akiingia ukumbini.
 Mwenyekiti akafungua sherehe kwa sara.
 Bonge la keki iliyotengenezwa na mama Semeo.
 Mama mkwe mtarajiwa akipokea keki.
 Wanakamati pia wakapewa keki kama shukrani kwa kufanikisha shughuli.
 Dada mkubwa Stella akigonga cheers.
 Mama Mugisha akatoa somo kuhusu unyumba,Namnukuu... Wanawake wengi wanakuwa wagumu wakiombwa, mpe hata akitaka mara tano, ndio kazi kubwa katika ndoa,,, Mwisho wa kunukuu.
 Mama mzaa chema nae akafunguka kwa mwanae, Nimekusomesha na sasa una dgree mbili, ya tat ni kumuhudumia mmeo.
 Mama akampa mwanae zawadi, na gari liko Dar atalikuta.
 Mmeo apendeze kuanzi kitandani, mwilini na mavazi, hizi hapa suti zake,,,,,
 Asantee mama, machozi yakawatoka ya furaha.
 KUSHOTO NI Mama mkwe wa Olivia akiwa na mama yake Olivia.
Mtu na dada yake, kila rakheri Olivia jamcobukoba. blogspot.com inakupongeza kwa hatua uliyofikia.

Sunday 8 November 2015

NI MWAKA MMOJA TANGU KAPTEN JOHN BARONGO AFARIKI NA MIAKA 10 TANGU MA WINFRIDA BARONGO AFARIKI,FAMILIA WAWEKA MISA.

Ni familia ya marehemu John Barongo wa Kanazi Bukoba vijijini katika picha ya pamoja baada ya ibada ya misa takatifu ya kuwakumbuka wazazi wao,mwaka mmoja wa kumaliza matanga ya marehemu baba yao Kapten John Barongo na miaka kumi tangu mama yao Ma Winfrida Barongo afariki,misa ilifanyika nyumbani kwa marehemu Kanazi Bukoba,katika uhahi wa marehemu Barongo amekuwa kiongozi serikalini na katika chama cha mapinduzi katika nafasi za juu.
Kaburi la Kapten John Barongo.
Kaburi la Ma Winfrida Barongo.
Mzee Pius Ngeze, mmoja wa wazee waliofanya kazi na marehemu akisalimiana na wanafamilia.
Mc Rutakwa akitoa maelekezo na mpangilio wa shughuli nzima.
Mzee Rutaraka rafiki mkubwa wa familia, akieleza namna walivyoishi na marehemu Barongo katika maisha yao ya harakati za kisiasa.
Baba mdogo akitoa nasaha kwa wanafamilia na wageni waalikwa.
Mtoto mkubwa wa kiume Gordwin Barongo akitoa neno la shukrani kwa wote waliofika kwa niaba ya familia.
Dada mkubwa wa familia akitoa neno na kuwashukuru wadogo zake namna wanavyomuheshimu na kupendana.
Kwaya ya BCC wakitumbuiza.
Joanitha Barongo akicheza na wanakwaya.
Lilian Barongo akiwa katika maeneo ya makaburi ya wazazi wake.
Gordwin Barongo akiwa maeneo ya makaburi.
Picha ya marehemu Barongo.
Wakati wa ibada.
Mkate wa bwana.
Pumzikeni kwa amani wazazi wetu.