Monday 9 November 2015

KITCHEN PARTY YA OLIVIA.T. KAIZA YAFANA KATIKA UKUMBI WA LINA'S BUKOBA.

 Kulia ni Bi harusi mtarajiwa anaetegemea kufunga pingu za maisha hivi karibuni  Bi Olivia .T. Kaiza akiwa na mama yake mzazi  Bibi Gozibeltha Evalista (Mama Stella) wakiwa  katika ukumbi wa Lina's, Wa mama Bukoba walimiminika wakiwa memependeza  na kumeremeta kwa ajiri ya kumfunda na kumtakia maisha mema ya ndoa, nasaha mbalimbali zilitolewa na wamama.
 Mama mzaa chema (kulia ) Mama Stella akiingia ukumbini.
 Mwenyekiti akafungua sherehe kwa sara.
 Bonge la keki iliyotengenezwa na mama Semeo.
 Mama mkwe mtarajiwa akipokea keki.
 Wanakamati pia wakapewa keki kama shukrani kwa kufanikisha shughuli.
 Dada mkubwa Stella akigonga cheers.
 Mama Mugisha akatoa somo kuhusu unyumba,Namnukuu... Wanawake wengi wanakuwa wagumu wakiombwa, mpe hata akitaka mara tano, ndio kazi kubwa katika ndoa,,, Mwisho wa kunukuu.
 Mama mzaa chema nae akafunguka kwa mwanae, Nimekusomesha na sasa una dgree mbili, ya tat ni kumuhudumia mmeo.
 Mama akampa mwanae zawadi, na gari liko Dar atalikuta.
 Mmeo apendeze kuanzi kitandani, mwilini na mavazi, hizi hapa suti zake,,,,,
 Asantee mama, machozi yakawatoka ya furaha.
 KUSHOTO NI Mama mkwe wa Olivia akiwa na mama yake Olivia.
Mtu na dada yake, kila rakheri Olivia jamcobukoba. blogspot.com inakupongeza kwa hatua uliyofikia.

No comments:

Post a Comment