Thursday 2 May 2013

DAYNA KUWASHA MOTO MISS MULEBA TAREHE 31.05.2013

Msanii wa nyimbo za kizazi kipya Dayna Nyange ambaye anatarajia kutoa burudani ya muziki kwenye Miss Redd's Muleba na wasanii wengine kibao tarehe 31.05.2013. Ambaye analetwa kwenu na Kareen Fashion na Point View Pub kushirikiana na Jamco Video Production. Siku hiyo ya tarehe 31.5.13 patakuwa  Hapatoshi Waisuka Hotel.
Karibuni sana...

COASTAL UNION YATIBUA SHEREHE ZA UBINGWA JANGWANI LEO, NA BAADA YA KUTOKA SARE YA 1-1


Mshambuliaji wa Yanga Jerryson Tegete akishangilia bao lake la pekee alillofunga kipindi cha kwanza akiwa na Said Bahanuzi na Nurdin bakari


Nizar Khalfan wa Yanga akiwa amebanwa vilivyo na mdogo wake Razack Khalfan wa Coastal Union kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa taifa, timu hizi zilitoka sare 1-1

Baadhi ya vikombe vilivyokuwepo uwanjani leo, hata hivyo vilishindwa kushehekewa vema baada ya Coastal Union kusawazisha


Mashabiki wa Yanga wakishangilia timu yao wakati ikipambana na Coastal Union ya Tanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara. Yanga tayari imetwaa ubingwa huo baada ya kufikisha pointi 57 ambazo hakuna timu yoyote inayoweza kuzifikia.