Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth
Magufuli wameungana na wananchi wa Rwanda kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 22 ya
tangu kutokea kwa mauaji ya kimbari yaliyosababisha vifo vya watu takribani
milioni 1.
Maadhimisho hayo
yamefanyika katika eneo la Gisozi Mjini Kigali, yalipo makumbusho ya mauaji ya
Kimbari ambapo Rais Magufuli na Mkewe wakiwa na mwenyeji wao Rais Paul Kagame
wa Rwanda na Mkewe Mama Janeth Kagame wameweka shada la mauaji katika eneo
walipouawa idadi kubwa ya wananchi wa Rwanda na pia wakawasha mwenge wa
matumaini kwa walionusurika katika mauaji hayo na kwa Taifa zima la Rwanda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Rwanda Paul Kagame wakiwasha mwenge
wa matumaini kuashiria kutotokea tena kwa mauaji ya Kimbari nchini Rwanda.
|
Pamoja na kupata
historia ya mauaji hayo ya kimbari, Rais Magufuli akiongozwa na mwenyeji wake
Rais Kagame ametembelea jumba maalum lililohifadhi kumbukumbu ya watu
waliopoteza maisha, ambapo amepata maelezo kutoka kwa wahifadhi wa makumbusho
hiyo, na pia kujioonea picha na mabaki ya mifupa na mafuvu ya binadamu
waliouawa.
Akizungumza mara
baada ya kutembelea jumba hilo la makumbusho Rais Magufuli ameelezea
kusikitishwa kwake na mauaji hayo na kusema tukio hilo halipaswi kurudia.
"Haitatokea
tena, hatuwezi kubadilisha yaliyopita lakini tunaweza kubadilisha mambo ya sasa
na yajayo, mauaji haya hayapaswi kutokea tena"
Amesema Rais Magufuli.
Wageni mbalimbali waliofika kwenye kumbukumbu hizo. |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia picha za watoto waliouwawa kinyama katika
eneo la Kumbukumbu ya Mauaji ya Kimbari
Gishozi Kigali nchini Rwanda.
|
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli akisaini Kitabu katika Jengo la makumbusho ya mauaji
ya Kimbari Gishozi Kigali nchini Rwanda.
|
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli akipokea kitabu chenye maelezo mbalimbali kuhusu
mauaji hayo ya kimbari.
|
Rais
wa Rwanda Paul Kagame akimpokea Rais Magufuli katika viwanja vya Gishozi kabla
ya kwenda kuweka mashada ya maua kwenye makaburi ya watu waliouwawa katika
mauaji ya Kimbari.
|