Thursday 4 January 2018

WAZIRI MWIJAGE: NJIA NZURI YA KUFIKIA UCHUMI WA KATI NI UCHUMI WA VIWANDA


Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe.Charles Mwijage akifungua Ofisi ya Muda ya Shirika la kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) iliyoko Mtaa wa Malambo mjini Bariadi wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe..Charles Mwijage akizungumza na wadau wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji wa Mkoa wa Simiyu wakati wa Ziara yake Mkoani humo
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe.Charles Mwijage(kulia) akisaini Kitabu cha wageni katika Ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Simiyu mara baada ya kufika hapo wakati wa ziara yake Mkoani humo (kushoto) ni Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe.Charles Mwijage akizungumza na wadau mara baada ya kutembelea eneo itakapojengwa Ofisi Mpya ya SIDO Isanga Mjini Bariadi, wakati wa ziara yake mkoani Simiyu.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe.Charles Mwijage (wa sita kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wadau wa viwanda Mkoa wa Simiyu wakati wa ziara yake mkoani humo.
Na Stella Kalinga, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage amesema njia nzuri ya kufikia Uchumi wa Kati ifikapo mwaka 2025 ni kupitia Uchumi wa Viwanda jumuishi.

Waziri Mwijage ameyasema hayo alipozungumza na wadau wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji wa Mkoa wa Simiyu wakati wa ziara yake Mkoani humo, ambapo alisisitiza juu ya Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda ulio imara, shindani na endelevu, utakayozingatia mambo muhimu matatu ambayo ni soko, malighafi na teknolojia.

Amesema lengo la Serikali ni kuhamasisha ujenzi wa Uchumi wa Viwanda Jumuishi ambao unawahusisha watu wengi kupitia viwanda vidogo na vya kati,vitakavyotumia malighafi zitakozozalishwa hapa nchini vilivyopo katika maeneo mbalimbali nchini, ukiwepo mkoa wa Simiyu ambao umeonekana kufanya vizuri katika eneo hilo.

“Safari ya Simiyu imeanza vizuri na lengo la safari ni kuhamasisha Watanzania kujenga uchumi wa viwanda jumuishi, viwanda ambayo malighafi yake inazalishwa na wananchi wenyewe, vitatoa ajira kwa wananchi walio wengi, vitatumia malighafi asilia na kutoa mazao yenye matumizi makubwa” alisema Mwijage.

Waziri Mwijage amepongeza juhudi zinazofanywa na Mkoa wa Simiyu katika Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda kupitia Falsafa ya “Wilaya Moja Bidhaa Moja Kiwanda Kimoja” ambapo sasa umejipanga kuelekea kwenye “Kijiji Kimoja Bidhaa Moja”.

Ameongeza kuwa mwaka 2018/2019 Serikali kupitia Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo(SIDO) litawasaidia wananchi kupata mafunzo ya ujasiriamali, uzalishaji na uchakataji, ambapo ameuhakikishia Viongozi wa Mkoa wa Simiyu kuwa Ujenzi wa Ofisi ya SIDO ya Mkoa huo eneo la Isanga Mjini Bariadi utakamilika kabla ya kuanza kwa vikao vya Bunge la Bajeti mwaka 2018, kwa kuwa fedha za ujenzi zipo.

Sanjali na hilo Waziri Mwijage amewataka Maafisa Ushirika kuwahamasisha wananchi kujiunga katika vikundi ili waweze kukopeshwa mitaji ya kuanzisha viwanda vidogo na Serikali pamoja na Taasisi nyingine za Kifedha kwa kuwa ni rahisi zaidi vikudi kufikiwa kuliko mtu mmoja mmoja.

Wakati huo huo Mwijage amewataka watendaji wote wa Serikali kuondoa vikwazo na kuacha urasimu unaoweza kuwakwamisha wawekezaji katika maeneo mbalimbali hapa nchini ili kuweza kuufikia Uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Akiwasilisha tarifa ya Mkoa, Katibu Tawala Mkoa Simiyu, Ndg. Jumanne Sagini amesema ili kuandaa mazingira mazuri yatakayowawezesha wawekezaji kuvutiwa na kuwekeza mkoani humo, wametenga maeneo ya uwekezaji na madawati ya uwekezaji kwa kila Halmashauri na timu mahsusi ya Mkoa ya kuanzisha na kuendeleza dhana ya Simiyu ya Viwanda inayoongozwa na Katibu Tawala Mkoa.

Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Mkoa wa Simiyu, Njalu Silanga amesema wako tayari kuunga mkono juhudi za Serikali kwa vitendo katika Ujenzi wa Viwanda vidogo na vya kati na akaomba Meneja wa SIDO Mkoa atembelee viwanda vilivyopo ili aweze kutoa ushauri juu kuboresha uendeshaji wa viwanda hivyo katika tija.

WANANCHI WAFURIKA USAJILI VITAMBULISHO VYA TAIFA MKOANI RUVUMA

Wananchi wakazi wa Kata ya Ndilima Mtaa wa Makambi Ndilima Wilaya ya Songea, wakikagua fomu zao kabla ya kwenda kwenye maalumu cha uchukuaji taarifa kwa maana ya kupigwa picha, uchuaji alama za kibaiolojia na saini ya Kielekrtoniki. Waliopo pichani ni Bi. Hadija Yahaya (mwenye gauni la Pinki kushoto) na Bwana Hussein Nyoni (Mwenye kofia kichwani) wote wakazi wa Mtaa wa Makambi Songea.
Hawa ni baadhi tu ya wakazi wa Kata ya Ndilima Wilaya ya Songea wakisubiri huduma ya Usajili Vitambulisho vya Taifa unaoendelea kwenye shule ya msingi ya Matogo na kuhusisha wananchi wote wenye umri wa miaka 18 na kuendelea. Kwa Wilaya ya Songea Kata zilizoanza zoezi ni Kata ya Ndilima na Seed-farm zoezi ambalo litafanyika wa siku saba tu kabla ya kuhamia Kata zingine za Wilaya hiyio.

Akionekana mwenye furaha ni Bi Haruna Thabiti Majwila wa Mtaa wa Makambi Ndilima mara baada ya kukamilisha hatua za usajili kwa maana kupigwa picha na kuchukuliwa alama za Kibaiolojia. Na hapa ya akiangalia muonekano wa Kitambulisho chake utakavyokua na kukagua picha yake kujiridhisha endapo picha yake imetoka vizuri. Kulia ni Afisa Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Bwana Agaton Magnus Komba.
Pichani ni Bwana Hausi Rashid Mamba akiweka saini yake ya Kielektroniki kwenye mashine maalumu ya uchukuaji alama za kibaiolojia( alama za vidole), picha na saini ya kielektroniki wakati wa zoezi la Usajili wananchi Vitambulisho vya Taifa linaloendelea katika Kata ya Ndilima wilaya ya Songea mkoani Ruvuma.
Bwana Michael Komba akikagua kwa makini (aliyevaa jezi) akikagua kwa makini taarifa zake zilizojazwa kwenye fomu ya maombi ya usajili kabda la kuingia kwenye chumba cha Usajili Vitambulisho vya Taifa. Zoezi la Usajili Mkoa wa Ruvuma limeanza rasmi tangu tarehe 02/02/2018 na linahusisha wananchi wote wa mkoa huo wenye umri wa miaka 18 na kuendelea.

Mamia ya Wananchi wa Wilaya za mkoa wa Ruvuma wamejitokeza kwa wingi kwenye vituo vya Usajili zoezi la Vitambulisho vya Taifa huku baadhi wakiwataka viongozi kusimamia utekelezaji wa agizo la Serikali la usajili Vitambulisho vya Taifa kuwa ni bure.

Wito huo umetolewa na wananchi wa Wilaya ya Songea wakidai kutozwa kiasi cha shs.2000/ za picha za kubandika kwenye kwenye fomu za utambulisho za Serikali za Mitaa wanakoishi na kudai gharama hizo ni kubwa kulinganisha na hali halisi ya maisha.

Hata hivyo Mwenyekiti wa Mtaa wa Makambi Bwana Anuari Methodi Nyoni ametolea ufafanuzi suala hilo na kueleza wananchi wanaoagizwa kuleta picha picha ndogo za passport size ni wale ambao wamekosa viambatisho muhimu vya kuwatambulisha na hivyo ili kujiridhisha kuwa mwananchi wanayemthibitisha kuwa ni mkazi wa eneo lao basi ni vema kuwa na picha yenye taswira yake ili kuepuka matumizi mabaya ya fomu za kuwatambulisha zinazotolewa na Serikali ya Mtaa.

Aidha amesisitiza Serikali yake ya Mtaa kusimamia na kutekeleza agizo la Serikali la kwamba zoezi la Vitambulisho vya Taifa ni bure na kusisitiza umuhimu wa wananchi kuelewa Serikali inaposema zoezi ni bure haina maana kwamba Serikali itafanya kila kitu; ikutolee copy viambatisho vyako au kukulipia gharama za picha hilo haliwezekani. Amesema wao kama wasimamizi wa zoezi hilo wanasisitiza mwananchi kufika kwenye kituo na picha yake au nakala ya viambatisho vyake na huduma nyingine zote mwananchi atazifuata mtaani zinazkotolewa.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi Hati Bi. Rose Joseph amesema Mamlaka ina mashine zake za kuwapiga picha wananchi na kwamba mwananchi anayefika kusajiliwa hapaswi kuja na picha ya passport size kama inavyoelezwa; ila changamoto kubwa ni kwa wale wananchi ambao hawana viambatisho vyovyote vya kuwatambulisha na wanahitaji kupata barua ya utambulisho wa Serikali za Mitaa wanakoishi. Hawa sasa kwa utaratibu waliojiwekea wenyewe barua za utambulisho zinazotoka kwenye Serikali za Mitaa na kugongwa muhuri wa Mtendaji au Mwenyekiti wa Mtaa wamekuwa na utaratibu wa kuweka picha ya mwananchi ili kujiridhisha na yule wanayemtambulisha kwetu.

Bi Rose amewasisitiza wananchi kujitahidi kuwa na viambatisho muhimu vinavyowatambulisha kuepukana na gharama zizisokuwa za lazima kwani mwananchi anayekuja kusajiliwa akiwa na cheti cha kuzaliwa, vyeti vya shule, Kadi ya kupigia kura, TIN namba, Leseni ya Udereva, Pasi ya kusafiria(Passport), Kadi ya Bima ya AFYA, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii au Kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi; vichache kati ya hivyo huyu mtu hahitaji barua ya utambulisho ya Serikali ya Mtaa kwani viambatisho vyake vinatosha kumtambulisha” alisisitiza

Amesema ni vema wafanyabiashara kutotumia Usajili wa Vitambulisho vya Taifa kama sehemu ya kujinufaisha na badala yake kutambua si wananchi wote wenye uwezo wa kulipa gharama za huduma wanazotoa na kuomba Mamlaka mbalimbali za Serikali kuangalia namna zinavyoweza kudhibiti changamoto hiyo ili wananchi wengi wajitokeze kwenye zoezi la Usajili wa Vitambulisho vya Taifa kwani zoezi hilo ni bure nala muhimu kwa kila mwananchi kushiriki.

Zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa limeanza mkoani Ruvuma kwa Wilaya za Nyasa, Mbinga, Songea, Namtumbo na Tunduru na linatazamiwa kumalizika mwishoni mwa mwezi wa tatu mwaka huu.

KHERI APOKELEWA MWANZA KWA KISHINDO.

Mjumbe wa Kamati kuu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Kheri D James kulia akisalimiana na Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Ndg:Anthony Dialo mara baada ya kuwasili katika ofisi za Ccm Mkoa wa Mwanza.
Mjumbe wa Kamati kuu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Kheri D James akiteta jambo na Mwenyekiti wa Ccm mkoa wa mwanza Dr. Anthony dialo.
Kaimu katibu mkuu wa Umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi Shaka Hamdu Shaka akizungumza na Wanachama wa CCM Mkoa mwanza katika Ofisi za CCM Mkoa wa Mwanza.
Mjumbe wa Kamati kuu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Kheri D James akizungumza na wanachama wa chama cha mapinduzi mkoa wa mwanza akielekea Uwasha wa CCM KIRUMBA.
Mjumbe wa Kamati kuu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Kheri D James akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Ilemela na Naibu waziri wizara ya Ardhi Dkt Angelina Mabula alipowasili katika mapokezi Uwanja wa CCM Kirumba
Mjumbe wa Kamati kuu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Kheri D James akisalimia na mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ilemela

Mjumbe wa Kamati kuu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Kheri D James akiwasalimia na wanachama wa chama cha mapinduzi na jumuiya zake Uwanja wa Ccm kirumba.
wanachama wa Ccm Wakipugia mikono

HAZINA SACCOS YATATUA CHANGAMOTO YA MIKOPO CHECHEFU (NON PERFORMING LOANS)

Meneja wa Hazina Saccos ambaye pia ni Katibu wa Bodi ya Chama hicho, Bw. Festo Mwaipaja (aliyesimama mbele) akiwapitisha wanachama katika taarifa ya utekelezaji kwa mwaka 2017 katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Hazina Saccos na ambaye pia ni Katibu wa Bodi ya Chama hicho, Bw. Festo Mwaipaja (katikati) akiwaelezea wanachama kuhusu riba inayotozwa na chama hicho ambayo ni nafuu ukilinganisha na taasisi zingine za fedha wakati wa Mkutano wa mwaka wa chama hicho uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam.
Wanachama wa Hazina Saccos wakifuatilia taarifa ya Chama chao katika Mkutano wa Mwaka uliofanyika katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango)

VYAMA vya kuweka na kukopa fedha (SACCOS) vimekuwa ni suluhisho la mikopo chechefu (non performing loans) kwa kutoa riba nafuu ukilinganisha na taasisi zingine za kifedha kama benki za kibiashara.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Hazina, Bw. Eligius Mwankenja alipokua akifungua mkutano wa mwaka wa Chama hicho Jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa chama hicho kinatoa riba ya kiasi cha asilimia 6.5 hadi 9 ilihali Taasisi nyingi za Fedha zikiwemo Benki hutoa riba ya zaidi ya asilimia 20 jambo linalochangia ongezeko la Mikopo chechefu.

“Hazina Saccos kwa kutambua kuwa watu wanaokopa wengi hawana dhamana kama nyumba, ardhi na vingine, imeamua kutumia kigezo cha kubakiwa na 1/3 ya mshahara kama kigezo cha kupatiwa mkopo wenye riba nafuu” alifafanua Bw. Mwankenja.

Kwa upande wake Meneja wa Hazina Saccos ambaye pia ni Katibu wa Bodi ya Chama hicho Bw. Festo Mwaipaja, alisema kuwa chama hicho kipo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango na kinahudumia Wafanyakazi wa Serikali na taasisi zake.

Kutokana na uwezo mkubwa wa chama hicho kujiendesha kimetoa ajira kwa wafanyakazi 11 ambao wanatekeleza majukumu ya kila siku ya chama na pia kimekuwa kikipata faida na kutoa kodi kwa Serikali hivyo kuchangia katika pato la Taifa kwa ujumla.

Aidha Chama kinatarajia kufungua mradi mkubwa wa Kitega Uchumi maeneo ya Njedengwa Mkoani Dodoma kwenye eneo lililotengwa kwa ajili yauwekezaji zikiwa ni juhudi za kukuza mtaji na kuchangia maendeleo.

“Jambo linalo vutia katika chama hichi ni kuwa Mwanachama wa Hazina Saccos anaweza kuchangia Sh. 20,000 kila mwezi kwa muda wa miezi mitatu lakini akawa na uwezo wa kukopa zaidi Sh. milioni moja hadi milioni tatu pia tunatoa mikopo ya biashara kwa wanachama jambo ambalo ni suluhisho la mitaji hivyo kuchangia kukuza uchumi wa nchi”. alieleza Bw. Mwaipaja.

Vilevile kimetoa viwanja kwa bei nafuu katika maeneo ya Kigamboni kwa Sh. 6500 kwa mita ya mraba, Chasimba kwa Sh. 4000, Kiluvya Sh. 7500 na sasa kinatarajia kutoa viwanja Mkoani Dodoma katika Maeneo ya Ihumwa, Ngaroni na Nzuguni B.

Chama cha Hazina Saccos kilianzishwa mwa 1973 kikiwa na wanachama 250 lakini kwa sasa Chama hicho kina wanachama hai 5045.
You might also like:

WAZIRI MKUU AOMBOLEZA MSIBA WA MKE WA NAIBU WAZIRI KANGI LUGOLA


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimfariji Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Kangi Lugola kwenye msiba wa mkewe MarehemuKamishna Msaidizi wa Polisi Mary Lugola Gerezani Railyways Club jijinio Dar es salaam leo January 3, 2018. (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU )
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitia saini kitabu cha maombolezo alipofika Gerezani Railways Club jijini Dar es salaam leo January 3, 2018 kwenye msiba wa Marehemu Kamishna Msaidizi wa Polisi Mary Lugola aliyekuwa mke wa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Kangi Lugola aliyefariki jana. (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ,akitoa pole kwa wafiwa alipofika Gerezani Railways Club jijini Dar es salaam leo January 3, 2018 kwenye msiba wa Marehemu Kamishna Msaidizi wa Polisi Mary Lugola aliyekuwa mke wa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Kangi Lugola aliyefariki juzi tarehe 1/1/2018. (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ,akitoa pole kwa wafiwa alipofika Gerezani Railways Club jijini Dar es salaam leo January 3, 2018 kwenye msiba wa Marehemu Kamishna Msaidizi wa Polisi Mary Lugola aliyekuwa mke wa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Kangi Lugola aliyefariki juzi tarehe 1/1/2018. (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AAGANA NA GAVANA WA BENKI KUU YA TANZANIA (BOT) ANAYEMALIZA MUDA WAKE PROF. BENNO NDULU PAMOJA NA KUKUTANA NA GAVANA MTEULE WA (BOT) PROF. FLORENS LUOGA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) anayemaliza muda wake Profesa Benno Ndulu mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) anayemaliza muda wake Profesa Benno Ndulu mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Gavana mteule wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Profesa Florens Luoga aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na na Gavana mteule wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Profesa Florens Luoga mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Gavana mteule wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Profesa Florens Luoga wa kwanza (kushoto) pamoja na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) anayemaliza muda wake Profesa Benno Ndulu wa kwanza (kulia) mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na na Gavana mteule wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Profesa Florens Luoga wa kwanza (kushoto) pamoja na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) anayemaliza muda wake Profesa Benno Ndulu wa kwanza (kulia) mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) anayemaliza muda wake Profesa Benno Ndulu Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) anayemaliza muda wake Profesa Benno Ndulu Ikulu jijini Dar es Salaam.