Rais
Jakaya Kikwete amesema ni utovu wa nidhamu na ukosefu wa adabu
unaoonyeshwa na baadhi ya Watanzania kuwatukana, kuwadhihaki na
kuwakejeli waanzilishi wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere na
Sheikh Abeid Amani Karume.
Rais
Kikwete alitoa kauli hiyo juzi alipokuwa kwenye mahojiano maalumu na
wahariri wa baadhi ya vyombo vya habari (wa Mwananchi hawakuwapo) ya
kuadhimisha miaka 50 ya Muungano.
Kauli
hiyo ilikuwa ni jibu la moja ya maswali alilokuwa ameulizwa na
wahariri hao kuhusu matusi, kejeli na dhihaka ambazo zimekuwa
zinaonyeshwa na wajumbe wachache wa Bunge Maalumu la Katiba juu ya
waasisi hao wa Tanzania na wabunifu wakuu wa Muungano wa Tanzania.
“Ni
kukosa adabu na ni utovu mkubwa wa nidhamu kwa Mtanzania yeyote
kuwatukana, kuwadhihaki au kuwakejeli waasisi wa Taifa letu. Hawa ni
watu ambao waliifanyia nchi yetu mambo makubwa,” alisema Rais Kikwete
na kuongeza:
No comments:
Post a Comment