Saturday 19 April 2014

PILIKAPILIKA ZA PASAKA BUKOBA,WAFANYABIASHARA WA VYAKULA WAUZA,UPANDE WA MAVAZI WENGI NENO HALI MBAYA LATAWALA.

 Ikiwa kesho ni sikukuu ya  Pasaka, Mwokozi  yesu kristo alieteswa na kufa msalabani kwa ajili ya mwanadamu inasherekewa duniani kote, Katika Manispaa ya Bukoba watu wengi  wameonekana barabarani wakipitapita huku na kule kwa ajili ya manunuzi na maandalizi ya Pasaka.Camera yetu ilipita maeneo mbalimbali na kujionea hali halisi, wengi wa wafanyabiashara wa vyakula wameonekana kuwa na furaha na kusema kuwa wanashukuru mungu biashara zao zimekwenda vizuri, huku wafanyabiashara wa nguo kulalamika na kusema  biashara si nzuri inaonekana ukata umetawala.
 Maeneo ya soko kuu kwa muuza viatu anasema biashara  si nzuri
 Dada Doro anasema mauzo si makubwa kama alivyotegemea
 Mama huyu anasema biashara mbaya, anawakaribisha wenye matumbo makubwa wafike kibandani kwake soko kuu wanunue mkanda wa kupunguza tumbo
 Mama Hawa Hasani akiwa katika manunuzi ya vyakula
 Watu kibao soko kuu
 Pilikapilika soko kuu
 Viungo
 Vyakula kibao
 Gozbart akifanya manunuzi
 Mama Achi na swaiba wake
 Maduka ya nguo majanga
 Mama Visram  katika hekaheka za Pasaka, mvua kubwa sana zimenyesha Asubuhi
 Ni furaha wakiwa kwenye maandalizi ya pasaka
 Dada Unice akiwa na Dada Enjoey
 Sadati akiwa dukani kwake
 Kijana Veda Mtaani
Jamcobukoba.blogspot.com tunawatakia Pasaka njema

No comments:

Post a Comment