Monday 25 May 2015

BURIANI MZEE SAMWELI NTAMBALA LWANGISA,AFARIKI DUNIA HUKO NEW YORK MAREKANI.

 Mwanasiasa mkongwe katika nchi ya Tanzania na muasisi wa chama cha mapinduzi  Mzee Samwel Lwangisa ameaga dunia leo majira ya saa tano asubuhi kwa saa za marekani,kwa hapa kwetu  ni saa kumi na mbili jioni.kwa mujibu ya maelezo ya mwana familia Bw Majid Kichwabuta taratibu  na mipango ya kusafirisha mwili  zinafanyika na taarifa rasmi zitatolewa, akiongea kwa njia ya redio Kasibante Mbunge wa jimbo la Bukoba Mjini Balozi Khamis Kagasheki ametoa pole kwa ndugu , jamaa na wanajimbo wote kwa kumpoteza kiongozi ambae anahistoria kubwa katika Taifa la Tanzania, Marehemu alikuwa kwenye matibabu nchini Marekani.
 Katika picha ni hivi karibuni  mwezi mmoja uliopita Mh Kagasheki alimtembelea  marehemu akiwa New york Marekani.
 Marehemu akiwa na mwanae Murungi  huko Marekani.
Mzee Lwangisa ni miongoni mwa viongozi wa kwanza waliofanya kazi na mwl Nyerere akiwa mkuu wa Mkoa wa kwanza wa Ziwa magharibi kwa sasa Mkoa wa Kagera. Bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihidimiwe.

No comments:

Post a Comment