Monday 15 June 2015

KATIKA KUTEKELEZA AGIZO LA RAIS LA UJENZI WA MAABARA,DIWANI WA KATA YA KASHENYE KANYIGO AANDAA HARAMBEE.

 Mh Diwani wa kata ya Kashenye Kanyigo wilaya ya Missenye Omurangira Adeodatus Rugaibura akisoma taarifa ya kata kwa kipindi cha 2010-2015,ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi.Mh Diwani aliandaa harambee kwa ajiri ya ujenzi wa maaabara ya shule ya sekondari Kashenye,Viongozi,wananchi wa eneo hilo wanaoishi na wasio ishi walishirikishwa,zaidi ya kiasi cha 80 milioni kinahitajika kukamilisha ujenzi wa maabara.
 Mwl Maburuki(kushoto) na mwenzake walishiriki tukio la kihistoria.
 Wadau wa maendeleo kata Kashenye.
 Wananchi waliojitokeza.
 Zoezi la harambee likiendelea.
 Bw Matunda nae akachukua mic kutangaza alichonacho.
 Ujumbe wa Bw Divo nao ulikuwepo.
Wa pili kulia ni Balozi Diodorus Kamala ambae amewahi kuwa mbunge wa jimbo  la Nkenge(na safari hii anatarajia kutangaza nia) nae alichangia mifuko hamisini ya saruji,Bw Julius rugemarila  ambae nae ameshatangaza nia ya kugombea(alituma mwakilishi, na Bw Kyombo ambae nae ni mgombea nae alichangia.Zaidi ya milioni 11 zilikusanywa ikiwa bado marengo hayajakamilika, kupitia jamcobukoba.blogspot.com inatoa wito wadau wote wa elimu wa ndani na nje kuchangia maabara kwa nia ya watoto wetu wapate elimu bora,zikiwa zimebaki siku chache kabla ya tarehe ya mwisho kufika utekelezaji wa agizo la rais Kikwete.

No comments:

Post a Comment