CCM Kagera yawafukuza madiwani wake 8
Katibu wa CCM mkoa wa Kagera Bw Avelin Mushi amemaliza Press Conf hivi
punde na kufafanua kuwa kikao cha Halmasahuri Kuu ya mkoa wa Kagera
imemaliza kikao chake hivi punde na kuamua madiwani 8 wa Manispaa ya
Bukoba kufukuzwa katika chama na kufutiwa nyadhifa za udiwani kutoka na
mgogoro uliokuwa ukiendelea.
Waliofukuzwa ni:
1. Richard Gaspar (Miembeni )
2. Murungi Kichwabuta (viti maalum)
3. Alexander Ngalinda ambaye pia ni Naibu Meya (Buhembe)
4. Yusuf Ngaiza ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa wilaya (Kashai)
5. Deusdedit Mutakyahwa (Nyanga)
6. Robert Katunzi (Hamugembe)
7. Samwel Ruhangisa (Kitendaguro) na
8. Dauda Kalumuna (Ijuganyondo).
Katibu huyo ameongeza kuwa madiwani hao wanaweza kukata rufaa kwa ngazi
za juu za chama wakiona hawakutendea haki na kuwa ngazi ya mkoa ina
mamlaka ya kufanya hivyo kwa madiwani wa ngazi hizo.
Aidha amesema kwa Bw Yusuph ngaiza ambaye ni mwenyekiti wa CCM
bukoba,nafasi yake hiyo inasubiriwa ngazi za juu ambazo ndizo zenye
mamlaka juu yake(kwa cheo hicho)
Manispaa ya Bukoba ina kata 14 na kati ya hizo kata 4 zinaongozwa na CDM(2) na CUF(2) hivyo kwa Bukoba mjini CCM imebakiza madiwani 3 TU wa kuchaguliwa .kama ifuatavyo
1.Kashai-Amefukuzwa
2. Miembeni-Amefukuzwa
3.Miembe-Amefukuzwa
4.Nyanga-Amefukuzwa
5.Hamugembe-Amefukuzwa
6.Kitendaguro-Amefukuzwa
7.Ijuganyondo-Amefukuzwa
8.(1)Kagondo-Amebaki (CCM) (Meya Amani)
9.(2)Nshambya-Amebaki(CCM)
10.(3)Kahororo-Amebaki(CCM)
11.Bilele-Amebaki(CUF)
12.Kibeta-Amebaki(CHADEMA)
13.Bakoba-Amebaki(CUF)
14.Rwamishenye-Amebaki(CHADEMA)
Hatua iliyochukuliwa ni nzuri katika kuhakikisha amani inatawala kwa mstakabali wa maendeleo ya manispaa yetu. Lakini mikakati gani imewekwa ya kichama kuhakikisha kuwa uwakilishi wa wananchi unaendelea? Hizo kata ambazo madiwani wamesimamishwa uwakilishi na utetezi wao katika balaza la madiwani ambapo mambo ya msingi yanayohusu kata husika yataelezwa na nani? Na je, hatua iliyochukuliwa wananchi wa kata husika wameelezwa kinaganaga kuhusiana na swalahili?
ReplyDeleteNi vyema maamuzi kama haya yanaenda kufanyika 'plan B' inaelezwa wazi!
Ifahamike swala la maendeleo si la kichama na halifungamani na itikadi za kichama bali ni uzalendo na moyo wa kulitumikia taifa kwa ustawi wa jamii zetu.