Thursday, 13 June 2013
KAGASHEKI CUP 2013 KUANZA 29-6-2013 KATIKA UWANJA WA KAITABA
Kagasheki cup 2013 inatarajiwa kulindima 29-06-2013,ligi hiyo inayodhaminiwa kwa asilimia mia moja na mbunge wa jimbo la bukoba mjini na waziri wa maliasili na utalii balozi khamis kagasheki, kwa mujibu wa mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya kagasheki cup,marick tibabimare ambae pia ni mwenyekiti wa chama cha mpira bukoba mjini amesema timu zitakazoshiriki ni za kata zote 14 za jimbo la bukoba mjini na amewataka viongozi wa timu kata zote 14 siku ya jumamosi wakutane katika uwanja wa kaitaba ili waweze kupewa taratibu za maandalizi ya kagasheki cup 2013,katika ligi ambayo uleta hamasa kwa wanajimbo la bukoba mjini ni kagasheki cup,na hii inatokana na maandalizi ambayo ufanyika na zawadi nono ambazo hutolewa na mh kagasheki, kwa ligi iliyokwisha mh kagasheki alitoa zawadi ya mshindi wa kwanza alijinyakulia kitita cha shilingi milioni tano,wa pili milioni tatu ,na watatu milioni mbili na nusu,lakini pia mh kagasheki hutoa jezi,viatu na mipira kwa timu zote .lakini pia mh kagasheki ugharamilkia gharama zote za uendeshaji wa timu ,kama posho za waamuzi,maji kwa ajili ya timu zote na gharama za uendeshaji uwanja na ndio maana wananchi wote uingia bure kuangalia mechi.timu zinazotarajiwa kushiriki ni bakoba mabingwa watetezi,kashai,miembeni,kitendaguro,ijuganyondo,bilele, zingine ni nyanga,kibeta,kahororo,hamugembe, rwamishenye,kagondo,nshamya na buhembe. kwa upande wa zawadi kagasheki cup mwaka huu zitatangazwa muda mfupi kuanzia sasa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment