Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa
Jamii Dr. Seif Rashid na Balozi wa Italia nchini Pierluigi Velardi
wakizindua maabara ya kisasa kwenye majengo ya Taasisi ya Afya ya
Ifakara (IHI) huko Bagamoyo hivi karibuni. Maabara hiyo ambayo ina
uwezo wa kutambua magonjwa mapya na yale ya hatari sana ikiwemo Ebola
bila kuhatarisha maisha ya watafiti inajulikana kitaalamu kama Biosafety
Lab 3, na ni ya kwanza ya aina yake katika eneo la Afrika Mashariki na
Kati. Maabara hiyo yenye thamani ya Shilingi bilioni 1.2 imejengwa kwa
ufadhili wa Serikali ya Italia na inasimamiwa na Taasisi ya Afya ya
Ifakara (IHI).
No comments:
Post a Comment