Wednesday 10 September 2014

RAIS WA UGANDA YOWERI KAGUTA MUSEVEN AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU MOJA


 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kwa ziara ya kikazi ya siku moja.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho kikwete akimtambulisha kwa Rais Museveni Mkuu wa Majeshi ya Tanzania Jenerali Davies Mwamunyange muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kwa ziara ya kikazi ya siku moja.Kushoto ni Inspekta Jenerali wa Polisi Ernest Mangu.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda wakikagua gwaride la Heshima lililoandaliwa na jeshi la Wananchi wa Tanzania.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Yoweri Museveni wa Uganda wakifurahia ngoima za utamaduni.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha ikulu jijini Dar es Salaam Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda na kufanya naye mazungumzo.Rais Museveni yupo nchini Tanzania kwa ziara ya kikazi ya siku moja.

No comments:

Post a Comment