Thursday 25 June 2015

JANUARY MAKAMBA APATA WADHAMINI 8024 KAGERA,APOKELEWA KWA SHANGWE BUKOBA MJINI NA KUELEKEA UJOMBANI MISSENYE.

 Naibu waziri wa  mawasiliano, sayansi na Teknologia January Makamba akiwa ameambatana na mkewe amewasili katika Mkoa wa Kagera na kupokelewa na mamia ya wananchi katika manispaa ya Bukoba na badae kuelekea wilaya ya Missenye ambako shughuli ya kudhaminiwa ilifanyika.Akiongea kwa nyakati tofauti katika Manispaa ya Bukoba na wilayani Missenye January Makamba amesema ametafakari sana kabla ya kuchukua fomu ya kugombea urais,amesema rais anaetakiwa kwa sasa kwa watanzania ni rais ambae anafikira mpya, mtazamo mpya na ambae anajua matatizo ya wananchi na anaetambua kuwa sasa inatakiwa Tanzania mpya.Mh January amepata wadhamini 8024 katika wilaya ya Missenye.
 Akiwasili uwanja wa ndege Bukoba.
 Akiwa na mkewe.
 Msafara ukiongozwa na pikipiki kuelekea ofisi za chama Bukoba mjini.
 Umati mkubwa Bukoba mjini
 Mwenyekiti wa uvccm Mkoa Kagera Yahaya Kateme akiwa na January Makamba.
 Katibu wa ccm Mkoa wa Kagera akimkaribisha.
 Mkewe akisalimia wananchi.
 Missenye.
 Mto Kagera.
 Akiwasili Missenye.


























 Mama mzazi wa January Makamba mwenye miwani akimkaribisha mwanae ujombani baada ya kudhaminiwa katika wilaya ya Missenye.



No comments:

Post a Comment