Sunday 21 June 2015

COSAD YAZIDI KUSAIDIA MAMBO YA KIJAMII,SASA KUKARABATI BAADHI YA MAJENGO YA SHULE YA MSINGI KITEYAGWA.

Cosad ni shirika lisilo la serikali ,makao makuu yake yapo nchini Marekani na kwa Tanzania makao makuu yapo Mkoani Kagera katika Manispaa ya Bukoba chini ya mkurugenzi mtendaji Bw Smart Baitan.Cosad imekuwa ikishughurika na kusaidi jamii katika mambo mbalimbali ya wananchi wake kwa waume kujikwamua katika wimbi la umasikini na kukuza kipato,Lakini  pia Cosad imekuwa ikisaidia katika swala zima la elimu,ikiwa ni pamoja na kuwapatia wanafunzi mambo muhimu ili waweze kupata elimu kwa kiwango cha ubora.Moja ya shule ambayo imekuwa ikinufaika na misaada mbalimbali ni shule ya msingi  Kiteyagwa iliyoko katika kata ya Kagondo, Mkurugenzi wa Cosad Bw Smart Baitan amesema ameanza toka mwaka 2003 kusaidia mambo mbalimbali katika shule ya Kiteyangwa ,amesema kuwa anajisikia faraja na fahari kubwa kuona cosad imeweza kuweka maktaba nzuri na ya kisasa kwa ajili ya wanafunzi kujisomea,kipo kituo cha jamii(COMMUNITY RESOURSE),Cosad wameweka umeme katika shule,wamevuta maji na kuweka thamani za ofisi,wamekuwa wakitoa scholarship,wamekuwa wakipeleka watu mbalimbali Marekani kwa ajili ya kujifunza baadhi ya mambo,na akatolea mfano wa Diwani wa kata ya Kagondo Anatory Aman alibahatika kupata fursa ya kwenda marekani kwa kulipiwa gharama zote na Cosad,Pia Cosad inafanya kazi za kijamii katika wilaya za Muleba na Karagwe kwa kusaidi vikundi mbalimbali katika ufugaji wa mbuzi wa kisasa.Kwa mwaka 2015 Cosad watakarabati ofisi ya mwalimu mkuu wa Kiteyagwa kwa kuitengeneza kisasa kwa kuweka vigae, mabati mapya nk,(katika picha ni walimu na  wanafunzi kutoka Marekani wakiwa shule ya msingi Kiteyagwa.)
Ni Baadhi ya majengo ya shule.
Kituo cha jamii.
Wanafunzi wakiwaimbia wageni.
Mkurugenzi wa Cosad Bw Smart Baitan akiwa na mwanae.
Mwalimu mkuu.

No comments:

Post a Comment