Wajumbe
wa Mkutano kati ya Mujata na makamu Mwenyekiti wa CCM Philip Mangula
wakifuatilia kwa makini Risala inayosomwa na Katibu wa Mujata Uswege
ASASI ya Muungano wa Jamii
Tanzania(MUJATA) imekishauri Chama cha Mapinduzi (CCM) mambo yanayochangia
kudhoofisha Chama na kutoa mwanya kwa vyama vya upinzani kupata nguvu na
kukubalika katika jamii tofauti na ilivyokuwa mwanzo.
Ushauri huo ulitolewa na Asasi hiyo
kwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Philip Mangula katika mkutano wake
na Wanachama wa Mujata uliofanyika katika ukumbi wa CCM Mkoa wa Mbeya uliopo
Sokomatola Jijini hapa.
Akizungumza katika mkutano huo
Mwenyekiti wa Mujata, Chifu Shayo Soja Masoko, ambaye alimwambia Makamu
Mwenyekiti kuwa Chama kikitaka kuendelea kutawala na kukubalika katika jamii
jinatakiwa kufanya utafiti kabla ya kuteua wawakilishi wa wananchi katika
maeneo mbali mbali.
Alisema Chama kikifanya utafiti wa mtu
anayekubalika katika jamii bila kujali uwezo wake wa kifedha na elimu na
kumchagua kuwa mwakilishilishi wao itasaidia kuondoa makundi, Rushwa na vurugu
katika jamii kutokana na makao makuu kuteua watu wasiokubalika na jamii.
Aidha katika Risala yao kwa Makamu
Mwenyekiti, Mujata walitoa maoni mbali mbali ya namna ya kukijenga chama na
kuendelea kuaminiwa na Watanzania ambayo ni pamoja na Chama kuwapa uongozi
ndani ya chama baadhi ya watu wanaoshindwa kuhoji utendaji wa Serikali kwa
ngazi za uenyekiti na katibu katika ngazi ya Shina.
Pia walishauri chama kudhibiti baadhi ya
wagombea wanaotumia fedha ili kupata madaraka hata kama hawakubaliki katika
jamii na uongozi kuendelea kuyafumbia macho bila kuwachukulia hatua zozote na
kufanya nchi kukithiri kwa rushwa.
Akijibu baadhi ya mambo yaliyoko kwenye
Risala hiyo, Makamu Mwenyekiti wa Tanzania Bara, Philip Mangula, alisema Chama
kina utaratibu wake wa kushughulikia wanachama wanaokiuka kanuni za chama kwa
maksudi kwa kuwaita na kuwaonya kwa misingi ya Katiba ya Chama.
Alisema katika Siasa hakukosekani
Machangudoa kamawalivyo mitaani ambao kazi yao ni kujipisha pitisha bila kujali
utaratibu na kuongeza kuwa jamii inatakiwa kuwadharau kabisa na kwamba hata
chama hakikubaliani na hali hiyo.
Mangula alisema Wanasiasa duniani kote
ndiyo waanzilishi wa migogoro katika jamii kutokana na kukosa Sera za
kuwaambia wananchi wake hivyo kulazimisha kuonekana kwa kutumia njia
zisizohalali ikiwemo kuwachonganisha wananchi.
Aliongeza kuwa wanaotafuta uongozi kwa
kutumia fedha ni halali kwamba hawana uwezo na hawajiamini ndiyo maana huna
mbinu mbadala ya kulamisha kukubalika ni kutumia fedha jambo ambalo linazalisha
taswira mbaya katika Taifa.
Aidha Mangula ambaye katika Mkutano huo
alivisha Shuka kama ishara ya kuwa Mlezi wa Chama cha Jamii popote nchini,
alikipongeza chama hicho kwa jinsi walivyofanikiwa kuzima baadhi ya matukio ya
uhalifu Mkoani Mbeya na kuondoa dhana mbaya iliyokuwa ikijulikana kuhusu Mkoa
wa Mbeya.
Baadhi ya mambo waliofanikiwa kudhibiti
na kuyakomesha kabisa ni pamoja na Uchunaji wa Ngozi, Mauaji ya Watoto, Upigaji
wa nondo, wananchi kujichukulia Sheria mikononi, Maandamano yasiyokuwa na tija
katika jamii, Vurugu zinazochochewa na vyama vya Siasa na viongozi wa dini
likiowemo suala la Uchinjaji wa Nyama.
|
No comments:
Post a Comment