Mwenyekiti wa chama cha Chadema Freeman Mbowe akiwasili kwenye uwanja wa Uhuru Platfom
Umati wa watu ukimpokea mwenyekiti wao, na wengine wakiwa wamekuja kushuhudia kwa macho Edickopta ikishuka uswahili viwanja vya mayunga
Bw Mweyunge akiweka mambo sawa uwanjani
Wapenzi nguri wa chadema wakiwa na furaha
Bw Kipara akisalimia wananchi
Mchungaji Mulaki Diwani wa kata ya Kibeta akitoa neno na kunukuu maneno katika Biblia
Edikopta ikiwa angani kabla ya kutua, ilizunguka maeneo kadhaa ya mji wa Bukoba
Wananchi wakiiangakia Edukopta ikitua
Mwenyekiti wa Chadema Taifa akiomba kabla ya mkutano kufunguliwa
Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Kagera Wilfred Rwakatare akifungua mkutano
Mbunge wa Arusha Mh Lema akiongea na wananchi
Mh Lema amezungumzia swala la Zito Kabwe kuwa amekuwa akihujumu chama kwa muda mrefu, na sasa wamefika mahara wameamua kufanya maamuzi ya kumvua nyazifa zote katika chama na atabaki na unge wa mahakama.
Mh Mnyika ameongelea swala la gharama za umeme kupanda na mikataba mibovu inayoliingiza Taifa kwenye hasara kubwa na wananchi kuwalazimu kuwa na maisha magumu
MH Mbowe pamoja na kuongelea maswala ya kitaifa, likiwemo swala la rasimu ya katiba na serikali tatu kuwa ndio msimamo wa Chadema na kuwaomba wananchi kuwaunga mkono kwa nguvu zote, na hasa wanapokwenda kwenye bunge hili,Pia amezungumzia swala la ubadhilifu uliotokea kwenye Manispaa ya Bukoba wa zaidi ya bilioni mbili, Mh Mbowe amesema na kawataka wananchi wa Bukoba na maeneo mengine kukubali ukweli na kupongeza viongozi wanaosimamia haki za wananchi hata kama si wa vyama vyao,(JAMANI MNYONGE MNYONGENI HAKI YAKE MPENI Nawapongeza sana madiwani wa ccm, chadema na cuf kwa kuwa kitu kimoja kusimama imara na hatimae CAG kutoa taarifa ya UFISADI WA ZAIDI YA BILIONI MBILI na kupelekea Anatory Aman kujiuzuru, ongereni sana.) Pia amewataka viongozi wa dini wasitumiwe vibaya na baadhi ya watu kuongelea sawala udini eti kwa sababu tu kiongozi furani amepatikana na na ufisadi au wizi lakini kwa kuwa ni dini tofauti anaonekana ni mwema wakati amehusika kuhujumu mali za wananchi na wizi.Amewaomba viongozi wa dini kukemea swala hilo na amesema kwa hapa Bukoba wapo watu sasa wameanza kugawa watu kwa udini ni hatari sana kwa kufanya hivyo.
Umati wa wananchi wakimsikiliza Mbowe
Dah jamaa ni balaaa
Ras akifurahia mkutano
Baada ya mkutano kwisha
No comments:
Post a Comment