Warembo
15 kati ya 30 wanaoshiriki shindano la Miss Tanzania 2014
walisindikizwa na mkali wa Bongo Fleva kutoka Jijini Dar es Salaam,
Tunda Man, katika kutoa burudani kali wakati wa shindano dogo la awali
la kumtafuta mrembo mwenye kipaji lililofanyika Babati Mkoani Manyara,
mwishoni mwa wiki. Pichani juu ni washindi wa tano waliofanikiwa kuingia
fainali ya shindano hilo la vipaji litakalofanyika jijini Dar es Salaam
baada ya wengine 15 kufanyika Arusha mjini.
Warembo hao walishindana vikali katika kucheza na kuimba miziki ya aina mbalimbali.
Jopo la majaji likifuatilia kwa makini shindano hilo
Kila aina ya stile za uchezaji zilioneshwa na warembo hao jukwaani...
Warembo wenzao waliobakia wakishangilia burudani ya vipaji kutoka kwa washiriki wenzao.
wadau wa sanaa ya Urembo Babati wakifuatilia shindano hilo.
Mkuu
wa Wilaya ya Hanang, Christina Mndeme aliye mwakilisha Mkuu wa Mkoa wa
Manyara, akiwa na waratibu wa show hiyo, Mzee Ally Sumaye (kushoto) na
Mfanyabiashara Mohamad Bajwa.
Msanii wa Bongo Fleva Tunda Man akitoa burudani kwa wadau wa urembo Babati.
Tunda Man aliburudisha vilivyo ukumbini hapo.
Ilikuwa ni shwangwe kwa warembo hao ambao wapo Mikoa yua Kaskazini kwa ziara ya kimafunzo katika hifadhi za Taifa.
No comments:
Post a Comment