Ni kawaida kumjulia hali mgojwa na kwenda kumpa pole pale anapokuwa hospital, Takriban miaka miwili iliyopita mama mzazi wa mfanyabiashara Ben Mulokozi alitokea Dar na kuja kumuona mama yake mzazi alie kuwa anaumwa na amelazwa katika hospital ya Ndolage ya Bukoba mjini inayomilikiwa na kanisa la kkkt,Bw Ben baada ya kufika hospital alimjulia hali mama yake na baada ya hapo alipita kila kitanda cha mgonjwa kumjulia hali na kujipatia pesa taslimu kwa ajili ya mlo wa siku mbili, hakika tukio hilo liliwapafaraja wagojwa na kufarijika sana na kuombewa dua nyingi,Ndugu msomaji leo tarehe 16-02-2016 mmiliki wa mtandandao huu nimepita katika hospital hiyo kumuona mgonjwa, kwa bahati nzuri nikakutana na mmoja mwa wagonjwa aliekuwa kalazwa kipindi hicho,lakini leo nae anamuuguza ndugu yake,mara baada ya kuniona akaniuleza kwa kihaya (omushaija ayatuale amaela abayo, omushule muno) YULE BW ALIETUPA PESA KIPINDI KILE YUPO, MSALIMIE SANA. Kwa kweli binafsi kuna kitu nikajifunza hapa kuwa WEMA HAUOZI,ni miaka miwili sasa imepita tangu afanye wema huo, lakini leo mtu anakumbuka.Hakika nimejifunza kitu.SWALI WEWE UMESAIDIA WANGAPI KATIKA NEEMA ULIZOJALIWA NA MWENYEZI MUNGU, Asanteeni.
Ben akiwa na mama yake hospital.
Hata wale waliokutwa kwenye bench wakisubiri kumuona daktari walipewa pesa ya mlo wa siku hiyo.
Ni wadau waliofika kumuona mgojwa wakiwa na Bw Ben aliesimama katikati.
Wakati muafaka ukafika wa kufungua .
Wagojwa wakitembelewa.
Wasibamu ota.
Mama ugua pole.
Zoezi la kupa mlo wa siku mbili likiendelea .
Picha ya pamoja.
Safari ya kurejea Dar.
No comments:
Post a Comment