Saturday 29 June 2013

NI KIVUMBI!! "REDDS MISS LAKE ZONE 2013" JIJINI MWANZA UKUMBI WA GOLD CREST HOTEL USIKU WA LEO!!

Ni kitimutimu cha Redd's Miss Lake Zone 2013 Kitakachofanyika leo Jijini Mwanza 29-06-2013 katika ukumbi wa Gold Crest Hotel,warembo watatu kutoka kila Mkoa katika mikoa sita ya kanda ya Ziwa watachuana kuwapata watatu ambao watakwenda kwenye mashindano ya Taifa, mbali na mchuano mkali utakaokuwepo, pia zitakuwepo burudani kutoka kwa Ommy Dimpoz na Michael Ross. ili uweze kushuhudia mtanange huu kiingilio cha kawaida ni Tsh20,000/= na VIP ni Tsh 40,000/=Washiriki wa redd's miss Lake zone 2013 wakifanya mazoezi yao ya mwisho leo kabla ya kuingia kwenye mtanange usiku huu.
Kinyang’anyiro cha kumpata Miss Kanda ya Ziwa kinatarajiwa kufanyika leo usiku katika ukumbi wa Gold Crest Hotel uliopo jijini Mwanza. Mratibu wa Shindano hilo Clara Mwassa, amesema baada ya warimbwende kutoka Mikoa yote inayounda Kanda ya ziwa na kukaa kambini tangu Juni 23, Mwaka huu na kupata mafunzo mbali mbali wanatarajia kuivunja leo hii Juni 29, Mwaka huu baada ya Mshindi kupatikana.


WASHIRIKI WA MISS REDD'S WAKIWA MAZOEZINILEO HII





Hakika kazi ipo leo usiku huu..

No comments:

Post a Comment