Sunday, 15 March 2015

HONGERA KAMANDA MWAIBAMBE NA TIMU YAKO NZIMA KWA KUKAMATA SIRAHA HARAMU .

 Ni Kamanda wa polisi Mkoa wa Kagera  Henry Mwaibambe akiwa naofisa upelelezi makosa ya jinai Mkoa wa Kagera Gilles Muruto wakiongea na waandishi wa habari,Baada ya kukamata Bunduki nne aina ya SMG,Risasi 129, Magazine sina na sare za jeshi za nchi jirani ya Burundi baada ya mapambano na majibizano ya risasi na majambaza katika pori la  Nyantakala wilaya ya Biharamulo na majambazi kutokomea na kukimbia.Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera walishirikiana na Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita.
Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali wakichukua matukio na taarifa ya kamanda Mwaibambe.
Mbali na tukio la kukamata siraha, pia Kamanda Herny Mwaibambe ameelezea matukio  ya mauaji  ya hivi karibuni katika kata ya Kitendaguro kuwa Polisi wanaendelea na uchunguzi na kuna baadhi ya watu wamekamatwa kwa ajili ya mahojiano,pia katika tukio la kuchoma makanisa mawili ya Kagondo na nshambya Kamanda amesema uchunguzi unaendele amewataka wananchi kutoa ushirikiano ili kuwabaini waarifu , na kusisitiza kuwa Jeshi la polisi linaendelea na msako mkali kuwakamata waalifu.
N siraha, risasi na sare za jeshi vilivyokamatwa.
jamcobukoba.blogspot.com inatoa pongezi  kwa jeshi la polisi kwa jitihada zinazofanyika kupambana na majambazi.

No comments:

Post a Comment