Tuesday, 15 October 2013

*RAIS JAKAYA KIKWETE ATOA ZAWADI YA EDI EL HAJJ KWA MAKUNDI MAALUM


 RAIS Jakaya Kikwete  msaada wa vyakula  wenye thamani ya Sh. milioni 5.5 kwa makundi maalum ambayo ni wazee  na wasiojiweza, watoto yatima na watoto walio katika  mkinzano na  kisheria kwa ajili ya kusherekea sikukuu ya Edi El Hajj.

 Msaada huo ulitolewa leo  kwa niaba ya Rais  Kikwete , na Kaimu Kamishna  wa Usatawi wa Jamii Rabirira Mushi   katika hafla fupi iliyofanyika kwenye mahabusu ya watoto iliyopo Regency  jijini Dares Salaam  kwa  vituo na makazi 12 ya makundi hayo yaliyopo hapa nchini.

“ Mhe. Rais  ametoa zawadi ya mbuzi, mchele na mafuta ya kupikia  ili kuona kwamba watoto na wazee hawa wanajumuika  na wanajamii wengine katika  sherehe hii,” alisema  Rabirira.

 Alivitaja vituo  vilipokea msaada huo kuwa ni  kituo cha watoto Dar  Al arkam na Nunge  vyote viko(Temeke), Msongola Orphaned  Centre(Ilala), Furaha(Kinondoni)  Mother Theresa(Mburahati), Malaika Kids Home(Mkuranga) na makazi ya wazee na wasiojiweza cha Kilima(Bukoba Vijijini).

Vituo vingine ni  Mahabusi ya watoto(Arusha Mjini), mahabusi ya watoto(Tanga Mjini), makazi ya wazeee Mwanzange(Tanga), makao ya watoto Istikana (Pemba ) na makazi ya wazee Sebuleni(Unguja).

Akizungumzia kuhusu msaada huo kwa niaba ya wenzake Mwenyekiti wa kituo cha Msongola Orphaned Trust Fund, Shanta Deus   alimshukuru Rais Kikwete kwa moyo wake wa kujitolea kwa  makundi hayo huku akiwataka watu wengine kuiga mfano.
“Ninawaomba watu wengine, sekta binfasi na kampuni mbalimbali kuiga mfano huu ili kuweza kuwasaidia watoto yatima na wanaoshi katika mazingira hatarishi pamoja na makundi maalum kwa kutoa misaada mbalimbali,”alisisitiza Shanta.

Naye Sista  Oliver  Paulo  ambaye ni mlezi wa  makao ya watoto ya yatima, kijiji cha Furaha  aliishauri jamii iwe tabia ya kushirikiana na makundi hayo katika sherehe mbalimbali na kuwasaidia.

No comments:

Post a Comment