Sunday 12 April 2015

DIWANI WA KATA KAGONDO ANATORY AMANI ANASHIKIRIWA NA POLISI RUMANDE KWA UCHUNGUZI WA UPOTEVU WA SIRAHA.

Aliewahi kuwa stahiki meya wa Manispaa Bukoba Dk Anatory Aman anashikiliwa na polisi  baada ya yeye kwenda kituo cha polisi kutoa taarifa ya  ya upotevu wa siraha yake (Pistol),Maelezo haya ni kwa mujibu ya mmoja wa wananchi tuliemkuta eneo la polisi Bukoba mara baada ya habari hizi kusambaa maeneo mbalimbali ya mji wa Bukoba, (chanzo cha habari hii) walishuhudia ndugu wa karibu na marafiki wa Dk Anatory Aman wakipita huku na kule kwa ajiri ya  kushughurikia dhamana,Jitihada za kumtafuta kamanda wa polisi Mkoa wa Kagera zinaendelea ili tuweze kupata undani  na ukweli wa jambo hili. Hivi karibuni Mji wa Bukoba umekuwa katika wimbi la wananchi kukatwa shingo na makoromewo katika baadhi ya maeneo, hali ambayo imewafanya wananchi kuishi kwa mashaka, lakini pia jeshi la polisi lipo linaendelea na operasheni ya kuyasaka majambazi yanayotumia siraha haramu kwa kuuwa wananchi na kuchukua mali zao.

No comments:

Post a Comment